Saturday, September 26, 2015


Tangazo la kukutana na kumpa pole Ndg. Abdul Mohamed Mpily (DJ Pred)Chama cha Watanzania Oslo
kinapenda kuwataarifu kuwa ndugu yetu Abdul Mohamed Mpily alimpoteza mama yake mpendwa Bi Fatuma Said Mwilola mnamo tarehe 31.08.2015 majira ya saa tano asubuhi kwa ajali mbaya ya gari maeneo ya Mbagala Mission,     Dar Es Salaam, Tanzania.

Abdul amekwisharejea na kama ilivyo desturi yetu, basi tungependa tukutane wote kwa kadri tutakavyoweza ili tuwe sote na ndugu yetu, wengi wetu hatukuweza kumpata baada ya ile tarehe 31.08.2015 kwani ilibidi awahi nyumbani kwa taratibu zote za mazishi na kuwa na familia yake kwa kipindi kigumu.

Tutakutana;

Siku: Jumamosi
Tarehe: 26.09.2015
Mahali: Masawa Pub Oslo.
Muda: saa kumi na mbili jioni (18:00  CET).

Wenu,
Daddy O. Hassan
Mwenyekiti,
Chama Cha Watanzania Oslo


No comments: