Sunday, February 18, 2018YAHUSU UTARATIBU WA MAOMBI YA PASIPOTI MPYA YA KIELETRONIKI YA TANZANIA KWA WAOMBAJI WA NDANI NA NJE YA TANZANIAUbalozi wa Tanzania Sweden umepokea maelezo toka Wizara ya Mambo ya Ndani, Idara ya Uhamiaji juu ya utaratibu wa maombi ya pasipoti mpya kama ifuatavyo:

"Idara ya Uhamiaji imeanza kutoa Pasipoti mpya za kielektroniki kwa Watanzania kuanzia tarehe 31. Januari 2018. 

Pasipoti za zamani zitaendelea kuwa halali kwa matumizi hadi ifikapo tarehe 31.Januari 2020. 

Utaratibu mpya wa maombi kwa sasa utawahusu waombaji wa pasipoti waliopo ndani ya nchi tu. 

Kwa waombaji waliopo nje ya nchi wataendelea na utaratibu wa zamani na kupewa pasipoti za zamani mpaka hapo mitambo ya kuchukua alama za vidole itakaposimikwa kwenye balozi zetu". 

Hivyo kwa taarifa hii watanzania mnaoishi nchi za Nordic na Baltic mtaendelea kutumia pasi mlizonazo na mkiomba mpya mtapata kama hizi za zamani mpaka hapo ubalozi utakapowezeshwa kupokea maombi ya pasi mpya.

Ukipata taarifa hii mwambie na mwingine!

MATIKU KIMENYA, 
KAIMU BALOZI 
UBALOZI WA TANZANIA 
NCHI ZA NORDIC NA 
ZA BALTIC, 
STOCKHOLM
SWEDEN.


No comments: