Monday, March 31, 2014
Saturday, March 29, 2014
It´s that time of the year again! From Wintertime to Summertime. Time conversion date Sunday 30th March 2014. Adjust the time from 02:00 to 03:00 Central European Time (CET)
Kuamkia Jumapili, 30.Machi 2014 hapa Norway na nchi za Ulaya Magharibi tunabadili majira, kutoka ya theluji kuingia ya Kiangazi. Kutokana na mabadiliko ya majira, tunasogeza saa moja mbele. Saa 8 za usiku hadi saa 9 za usiku. Tutapishana saa moja na saa za Afrika Mashariki
(EAT = East African Time).
(EAT = East African Time).
Mfano: Ikiwa CET ni saa 6 mchana, EAT ni saa 7 mchana.
Thursday, March 27, 2014
Malawi - Government on Tuesday said statement by political leaders legally binds agreements and that confirms Malawi's sole ownership of Lake Malawi.
Malawi´s Minister of Foreign Affairs, Ephraim Nganda Chiume was speaking in Lilongwe on the mediation meeting over the lake dispute held in Maputo, Mozambique on 20 to 21 March, 2014.
"Late President Julius Nyerere, Prime Minister Rashid Kawawa and former President Benjamin Mkapa informal comments were considered public statements for the record, depicting government's position on the matter, made after deliberation and review of historical and legal advice," explained Chiume.
He added that the statements were also not simply declarations against interest in the context of the Malawi-Tanzania dispute, but were motivated by Tanzanian concern at the time about its other borders more generally.
"The comments by Tanzania clearly show, therefore, that the issue engages important and detailed principles of international law that are relevant across the African continent, not simply for the Malawi-Tanzania dispute," he said.
The minister then said the High Level of Mediation Team (HLMT) told the meeting that the two countries had to look at the resources found in the lake, and to jointly come up with ways of optimally using and sharing the resources and that approach, the boundary issue would automatically fall in place and be easily resolved in the process.
"I explained Malawi's position that in as far as the matter is concerned, the fundamental issue is to determine first where the boundary lies. Who owns the lake and thereafter, the issue of resources that may found in the lake can be looked into," said Chiume.
The Minister said the issue of resources from the lake does not arise, since people from Tanzania have always had access to the lake, as provided in the Anglo-German Agreement of 1890.
The delegation at the meeting also further informed the HLMT that if hydro-carbon resources were found in the lake there was no way the country would have exploited these resources without involving Tanzania and Mozambique.
The minister then assured Malawians that the country has a sound case in law and confidence in the HLMT and believe that the dispute in question would be resolved amicably.
The HLMT then spelt out the importance of establishing the boundary first before considering how the resources in the lake can be shared after the Tanzanian counterparts also agreed on the establishment of the lake boundary before looking at the resources found in the lake.
The mediation team was meeting for the first time after the two countries has made submissions of their respective positions on the boundary at the beginning of 2013 and also submissions of the responses to the questions the HLMT had raised to the two countries.
The meeting was attended by former Presidents, Joacquim Chissano of Mozambique, Tambo Mbeki of South Africa, Festus Mogae of Botswana and high level team of Legal and Technical Experts that the HLMT engaged to advise on boundary, legal and ther related matters.
Copyright Malawi News Agency. Distributed by AllAfrica Global, 26.03.2014

Notice: Changes to the UK Visa application centre in Tanzania
NEXT GENERATION OUTSOURCED VISA (NGOV) PROJECT
PRESS RELEASE
Tanzania
25 March 2014
On 31 March, our new commercial partner for UK visa services, Teleperformance Ltd., will take over the running of our Visa Application Centre in Tanzania. The Visa Application Centre will be moving from its current location at the British High Commission to different premises in Dar es Salaam as follows:
New Teleperformance Application Centre Address
Viva Towers,
294-295 Ali Hassan Mwinyi Road,
Upanga,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Date of Relocation
31 March 2014.
UK visa customers will continue to complete their applications and pay their visa fee online at Visa4UK before selecting an appointment at the Teleperformance application centre. Hours of operation at the new centre will be increased from 0830-1630hrs, offering a wider range of daily appointments. Our standard service levels will not change as a result of outsourcing to a commercial partner. Operating outsourced Visa Application Centre facilities allows us more flexibility to drive improvements in customer service with greater access to added value services such as priority visas and return courier options. We will work closely with our commercial partner to ensure continuity of service during the transition period.
All UK visa applications will continue to be decided by UK Visas & Immigration staff.
The UK remains open for business and these new arrangements will allow us to maintain a world class, competitive visa system to support Britain in the global race. We are listening to the needs of our customers and these changes will improve our service by increasing the number of visa application centres globally and expanding the number of locations and countries where premium services are available.
Notes for Editors
The Next Generation Outsourced Visa (NGOV) Project will deliver the next set of outsourcing contracts for the UK visa application process, including biometric enrolment, courier services and interviewing facilitation. These will replace current contracts that are due to expire in March 2014. The new contracts will allow UK Visas & Immigration to:
Increase the number of application points globally, Offer improved customer services, including increased access to premium and priority services, and Deliver efficiencies in the visa application process.
Haki ya Watanzania kuzaliwa ughaibuni
Taifa letu likiwa katika mpito na wakati mgumu wa kuandika rasimu ya katiba mpya ya watanzania, hatuna budi kuweka kando itikadi zetu za kisiasa, tofauti za kiimani na hata maslahi binafsi ili tuungane katika kutafuta katiba itakayokidhi mahitaji yetu ya sasa na ya vizazi vijavyo.
Katika mchakato huu, inatubidi tuwe makini na wakweli katika kujadili hatma na haki ya kuzaliwa ya ndugu zetu ambao wanaishi ughaibuni. Lazima tuwajumuishe na kuwapa haki zao za msingi; haki ya kuzaliwa katika ardhi ya Tanzania ambayo ni zawadi kutoka kwa mwenyezi Mungu. Hii ni haki ambayo kamwe haiwezi kubatilishwa na mamlaka ya aina yeyote wala haiwezi kutenguliwa na binadamu yoyote. Ni kujidanganya kudai kwamba waliochukua uraia wa kigeni warudi Tanzania kama wageni.
Kwa makusudi kabisa, nimeamua kuchokonoa huu mjadala wa haki ya kuzaliwa nikiwa na sababu nyingi za manufaa kwa taifa letu; ya msingi ikiwa ni sababu ya kiuchumi na hatma ya taifa letu. Jamii ya watanzania wanaoishi ughaibuni ni hazina adimu ya rasilimali watu wanaohitajika katika maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ya Tanzania.
Ni kundi lenye uwezo mkubwa wa kiuchumi ambao lazima tuwakumbatie. Mheshimiwa Rais Jakaya kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waheshimiwa Dr. Wilibrod Slaa, Freeman Mbowe, Bernard Membe, wote, kwa kipindi kirefu wameunga mkono haki ya kuzaliwa ya watanzania wanaoishi ughaibuni kupata haki zao za msingi za kurudi katika ardhi yao ya kuzaliwa bila masharti wala vikwazo vya aina yoyote
Bila shaka wapo wanasiasa wenye ajenda zao binafsi ambao wamekuwa kikwazo kikubwa katika kuwazuia wazawa wa Tanzania wanaoishi ughaibuni kupata haki sawa katika katiba mpya. Siwezi kuwalaumu, kwani pengine wengi hawana uelewa wa faida ambazo zitapatikana kwa kuwapa ndugu zetu waliozaliwa Tanzania haki ya kushiriki katika ujenzi wa taifa.
Mjadala huu tuaouanzisha lazima uweke katika mizani faida na athari za kuwapa watanzania haki yao ya kuzaliwa na hatimaye kupata uwiano ambao utakidhi na kujibu maswali mazito ambayo ndio chanzo cha vikwazo vilivyopo kwa sasa.
Wiki chache zilizopita, Blogger-mwanasiasa mmoja nchini Tanzania alitoa shutuma dhidi ya watanzania wajulikanao kama wana Diasapora wanaodai haki zao za kuzaliwa katika ardhi ya Tanzania, huku akisahau kwamba yeye mwenyewe alikuwa mwana Diaspora kwa miaka takribani thelathini. Hata kama alikuwa na uraia wa nchi thelathini, mwisho wa siku alirudi katika ardhi aliyozaliwa yaani, Tanzania. Nina imani kwamba anao wanafamilia ughaibuni ambao ndoto yao kubwa ni kutambulika kama watanzania wenye haki zote ambazo kila mzawa anazo.
Katika tafsiri isiyo rasmi ni kwamba amewatosa ndugu zake. Warudi Tanzania wasirudi siyo tatizo kwake. Tofauti na mategemeo ya wengi, huyu blogger alitegemewa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha na kutetea haki za kuzaliwa za watanzania wanaoishi ughaibuni.
Huyu blogger ndio picha kamili ya wanasiasa ambao mara nyingi hutafuta nafasi za kupiga picha na wanadiaspora pindi wanapotembea nchi nyingine ambako kuna watanzania. Wanasiasa hawahawa watakuwa mstari wa mbele kujipanga uwanja wa ndege kuonyesha huzuni na huruma na hata kumwaga machozi ya kinafiki pale majeneza ya wana Diaspora yanaporudishwa katika ardhi yao ya kuzaliwa huku wakiwanyima haki zao za kuzaliwa wanapokuwa hai.
Wengi wa watanzania waliomba uraia wa nchi nyingine siyo kwamba hawalipendi taifa lao,la hasha! Wengi ni wazalendo waliolazimika kuchukua uraia wa nchi nyingine ili kupata ahueni kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili mamilioni ya watanzania. Wengine walitafuta vibali vya kuishi ili wapate elimu ambayo Tanzania isingeweza kuwalipia.
Badala ya kutafuta chimbuko la tatizo au wazo fulani, ni desturi yetu kama jamii kwa mjumbe kusulubiwa na hata kuuwawa ili kuliua wazo au jambo linalotishia maslahi ya wachache. Kumshambulia John Mashaka mathalani, hakutaweza kamwe kuliua swala ambalo wakati wake umewadia. Binafsi nimeamua kubaki na uraia wangu wa kitanzania licha ya kuwa na nafasi ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Kubwa ya yote, ninajikita kuanzisha huu mjadala ili kuitetea Tanzania na rasilimali zake hasa rasilimali watu.
Kama taifa, tunawahitaji ndugu zetu wenye taaluma mbali mbali waliotapakaa kote duniani na hata kufikia hatua ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Napigania watanzania milioni 45 nikizingatia faida za kiuchumi, kisiasa, kijamii ambazo zinapatikana na rasilimali watu wenye asili ya kitanzania. Wazawa wanaopigania haki zao za kuzaliwa pamoja na vizazi vyao.
Ni muhimu hawa wanasiasa wakakumbushwa kuhusiana na maamuzi yao ya kuwatenga watanzania walio nje ya nchi, hususan kuwanyima haki zao za kuzaliwa. Inabidi wakumbushwe kwamba, wazaliwa wa Tanzania wanaoishi ughaibuni wana ndugu zao Tanzania, ambao ndio wapiga kura wao. Na ikiwa wanaamua kwa makusudi kuwatenga, basi kundi hili maarufu kama Diaspora watumie uwezo wao, ushawishi wao na mbinu zote walizo nazo kuwaadhibu wanasiasa wanaozuia haki zao za kuzaliwa
Pengine niwakumbushie viongozi wa jumuiya za watanzania popote walipo duniani kwamba haki haiombwi. Haki inadaiwa, na asiyeweza kudai haki yake na hata kuiona haki yake kama zawadi au upendeleo fulani basi huyo amepoteza haki yake ya kuishi.
Viongozi wa jumuiya za watanzania ughaibuni hawana budi kuonyesha uwezo wao wa kuongoza kwa kuwa mstari wa mbele wakiwahamasisha watanzania waliotapakaa duniani kudai haki zao za kuzaliwa. Inabidi wapaze sauti zaidi ili viongozi wetu walioweka pamba masikioni wasikie madai yao. Mashabiki wa CCM ,CUF, CHADEMA na wengineo wote wataathirika sawa. Kwa maana hiyo, vita hivi havina mipaka, ni vita vya watanzania wa matabaka yote. Wana diaspora lazima wawe na mshikamano kama watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania
John Mashaka
mashaka.john@yahoo.com
Monday, March 24, 2014
Tanzania has said it was not breaking any law by negotiating the border dispute with Malawi on Lake Nyasa
By Assah Mwambene
Tanzania has said it was not breaking any law by negotiating the border
dispute with Malawi on Lake Nyasa, including the 1964 AU resolution on the need
by African countries to respect colonial borders, saying the AU clause did not
stop anyone from pursuing a justifiable dispute.
Foreign Affairs and International Cooperation
Minister Bernard MembeForeign Affairs and International Cooperation Minister
Bernard Membe.
Speaking at the end of the two-day meeting
organised by the African Forum of Former Heads of State and Government from the
SADC, the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr
Bernard Membe said claims by Malawi that Tanzania was against the resolution
was totally uncalled for.
He said The 1964 AU declaration, famously referred to as Nyerere
Doctrine on the Principle of State Succession, does not stop any country which
is in dispute with its borders to pursue the matter as Tanzania was doing.
“At the moment we have more than 21 cases at the AU on border disputes,
this signifies that countries must sit down and negotiate these issues. So the
1964 kind of declaration does not close the doors to resolve the border
disputes by peaceful means.”
On the claims by Malawi that Tanzania was going against the Father of
the Nation, Mwalimu Julius Nyerere, quoting him as confirming that Tanzania
does not hold even a drop of water in the lake Nyasa, the Minister said
Tanzania’s position, is established on the principle of international law that
unilateral statements made by senior political leaders are not legally binding
upon the parties in respect of dispute at hand.
He said for Malawi to rely on the principle would not help them make a
case since it was long established that in the border dispute like the one in
lake Nyasa can not just be resolved by a unilateral statement made by political
leaders.
He quoted a precedence established by the International Court of
Justice in the boundary dispute between Burkina Faso and the Republic of Mali
as it is reported in the ICJ reports of 1996 in para 40 is relevant in which it
was ruled that no grounds to interpret the declaration made by Mali’s Head of
State.
“Since no agreement of this kind of conclusion between the parties, the
chamber finds that there are no grounds to interpret the declaration made by
Mali’s head of state on the 11th of April 1975, as a unilateral act with legal
implication in regard to the present case,” The Minister quoted the report.
He said therefore, Tanzania position was that boundaries are not
affirmed by mere statements by senior government officials, saying they are
negotiated and agreed by way of treaties, saying negotiation was a mandatory
procedure.
Mr Membe was leading the Tanzania delegation to Maputo. He was
accompanied by the Minister for Lands, Housing and Human settlements
Development, Prof Anna Tibaijuka and the Attorney General, Frederick Werema.
Former Mozambican President, Joachim Chissano is leading the African Forum of
Former Heads of State and Government in the SADC, assisted by Thabo Mbeki of
South Africa and Festus Mogae of Botswana.
Source: Tanzania Daily News
Friday, March 21, 2014
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, WAKATI WA KULIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA, TAREHE 21 MACHI, 2014, DODOMA
Mheshimiwa Samuel
Sitta, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba;
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mheshimiwa Anne Semamba Makinda; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ;
Mheshimiwa Rashid Othman Chande, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Viongozi Wakuu Wastaafu;
Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba;
Waheshimiwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Pongezi
Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kunipa fursa ya kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge letu Maalum la Katiba katika siku hii muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu. Nimekuja kuwatakia heri na naungana na Watanzania wenzetu wote kuwaombea baraka za Mwenyezi Mungu, ili muweze kuifanya kazi yenu kwa utulivu, hekima, umakini mkubwa na kuimaliza kwa salama na kwa mafanikio yanayoyatarajiwa na Watanzania.

Natoa pongezi nyingi kwako na kwa Makamu wako
kwa kuchaguliwa kwenu kuongoza Bunge hili maalumu na la kihistoria. Ushindi
mkubwa mliopata ni kielelezo tosha cha imani kubwa na matumaini waliyonayo
Wajumbe wenzenu kwenu. Matumaini yao ndiyo matumaini ya Watanzania wote, kwamba
mtaliongoza vizuri Bunge hili, ili liweze kutimiza kwa ufanisi mkubwa jukumu
lake muhimu sana katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Niruhusu pia niwapongeze kwa dhati Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa bahati ya aina yake waliyopata ya kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fursa hii hutokea mara chache sana katika historia ya nchi yo yote na watu wake. Mkifanikiwa kuipatia nchi yetu Katiba nzuri majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu, katika kumbukumbu za historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni matarajio ya Watanzania kuwa mtatunga Katiba
itakayokubalika na wengi. Katiba inayotekelezeka. Katiba itakayoimarisha
Muungano wetu kwa kuondoa changamoto zilizopo sasa. Katiba itakayoipa nchi yetu
mfumo bora wa kuongoza na kuendesha mambo yetu. Katiba itakayoimarisha umoja,
upendo, ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Tanzania, licha ya
tofauti zao za asili za upande wa Muungano na maeneo watokako, au tofauti za
jinsia, rangi, kabila, dini na ufuasi wa vyama vya siasa. Katiba itakayodumisha
amani, usalama na utulivu nchini. Katiba itakayostawisha zaidi demokrasia, haki
za binadamu, utawala wa sheria, utawala bora na kudhibiti maovu.
Na, mwisho ingawaje siyo mwisho kwa umuhimu, Katiba itakayoweka
mazingira mazuri kwa uchumi wa nchi kukua, na wananchi wengi kunufaika sawia na
maendeleo yatayopatikana.
Historia ya Katiba Nchini
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe;
Hii itakuwa mara ya tatu tangu kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 26, 1964, kwa nchi yetu kuwa na mchakato wa kutunga Katiba mpya. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1965 ilipotungwa Katiba ya Muda na mara ya pili ni mwaka 1977 ilipotungwa Katiba ya Kudumu tuliyonao sasa. Tofauti na mara mbili zilizopita, safari hii mchakato unahusisha watu wengi zaidi. Wananchi wameshiriki moja kwa moja kutoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na ndio watakaofanya uamuzi wa mwisho kuhusu Katiba mpya kwa kura ya maoni. Wananchi pia walipata nafasi ya kuchagua Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yaliyojadili Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Pia walipata nafasi ya kutoa maoni yao kupitia Mabaraza ya Katiba ya taasisi. Katika Bunge hili wapo wananchi 201 kutoka makundi mbalimbali.

Katika mchakato wa kutunga Katiba za mwaka 1965 na 1977 kulikuwapo Tume
za Kuandaa Rasimu na Bunge Maalum la Katiba kama ilivyo katika mchakato huu.
Hata hivyo, kwa Katiba zilizopita Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pekee
ndio waliounda Bunge Maalum. Safari hii Bunge Maalum linajumuisha Wabunge,
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wananchi 201 wanaotoka kwenye jamii,
wakiwakilisha asasi na makundi mbalimbali ya Watanzania kutoka Zanzibar na
Tanzania Bara. Mchakato wa sasa utaishia kwenye kura ya maoni itakayoshirikisha
wananchi wote wa Tanzania wanaoruhusiwa kupiga kura. Michakato iliyopita
iliishia Bunge Maalum pekee.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tangu kutungwa kwake, tarehe 25 Aprili, 1977, mpaka sasa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko takriban mara 14.
Mabadiliko hayo yalitokana na kufanyika au kutokea kwa mabadiliko muhimu ya
kiuchumi, kisiasa na kijamii katika nyakati mbalimbali hapa nchini na katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa ruksa yako naomba nitaje baadhi ya mabadiliko
yaliyofanywa:-
1. Mabadiliko ya 1979 yaliunda Mahakama ya Rufani ya Tanzania kufuatia
kufa kwa Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki baada ya kuvunjika kwa Jumuiya
ya Afrika Mashariki mwaka 1977.
2. Mabadiliko ya mwaka 1980 yalifanyika baada ya kutungwa kwa Katiba ya
Zanzibar, hivyo kulazimu Katiba hiyo kutambulika kwenye Katiba ya Jamhuri ya
Muungano.
3. Mabadiliko ya mwaka 1984 yaliweka utaratibu wa ukomo wa vipindi vya
Urais ambao haukuwepo kabla ya hapo. Aidha, masuala ya Haki za Binadamu (Bill
of Rights) yaliingizwa kwa mara ya kwanza katika Katiba. Vilevile, Mahakama ya
Rufani ya Tanzania na mambo mengine ya iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
yaliongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano.
4. Mwaka 1992, yalifanyika mabadiliko yaliyoanzisha Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa badala ya ule wa Chama kimoja uliokuwepo tangu 1965. Pia utaratibu wa uchaguzi wa Rais na Wabunge ulirekebishwa ili uendane na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Vilevile utaratibu wa kuwa na viti maalum vya wanawake katika Bunge ulianzishwa. Wakati ule ilikuwa asilimia 15 ya Wabunge wote. Aidha, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Bunge lilipewa mamlaka ya kumwajibisha Rais na Waziri Mkuu kupitia kura ya kutokuwa na imani.
5. Mabadiliko ya mwaka 1994 yaliweka mfumo mpya wa kumpata Makamu wa Rais kupitia Mgombea Mwenza.
6. Mwaka 2000 na 2005, pamoja na mambo mengine yalifanyika mabadiliko yaliyopanua wigo wa Haki za Binadamu na kuongeza uwakilishi wa wanawake.
Umuhimu wa Mabadiliko ya Katiba

Kufanyika kwa mabadiliko hayo kunathibitisha utayari wa Serikali kufanya mabadiliko kila ilipoonekana inafaa kufanya hivyo. Pamoja na kufanya yote hayo na Serikali kuwa na msimamo huo, kumekuwepo na madai yaliyokuwa yanajirudia ya kutaka Katiba ya Tanzania iandikwe upya. Wako watu walioimithilisha Katiba yetu na nguo yenye viraka vingi mno kiasi kwamba ingefaa kununua mpya badala ya kuendelea kuivaa.

Madai ya kutaka Katiba mpya yalipazwa sauti
baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Wapo waliokuwa wanadai
Katiba mpya kwa imani, eti kwamba, itawawezesha kuishinda CCM. Lakini, si hayo
tu, hata katika mchakato wa Serikali zetu mbili kushughulikia kero za Muungano,
imedhihirika kuwa baadhi ya changamoto zilikuwa zinahitaji mabadiliko ya Katiba
ili kuzipatia ufumbuzi wa uhakika na wa kudumu.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa kutambua ukweli huo na baada ya kushauriana na kukubaliana na viongozi wenzangu wakuu wa Chama tawala na Serikali zetu mbili wakati ule, ndipo tarehe 31 Desemba, 2010, nikatangaza dhamira ya kuanzisha mchakato wa kutunga Katiba mpya.

Nilieleza siku ile kuwa katika mchakato huo
tutakuwa na ushirikishwaji mpana wa wananchi wa Tanzania kwa makundi yao ya
jinsia, dini, siasa na shughuli wazifanyazo kujipatia riziki na kwa maeneo
wanayotoka katika pande zetu mbili za Muungano.
Mchakato wa Katiba Mpya
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tarehe 16 Machi, 2011 Baraza la Mawaziri liliridhia kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya kuliongoza taifa katika mchakato wa kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tarehe 18 Novemba, 2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, mchakato wa kutunga Katiba Mpya ulikuwa unaanza kwa kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Tume hiyo imepewa jukumu la kusikiliza maoni ya wananchi mmoja mmoja na kwa makundi yao ya maslahi, taasisi zao na kupitia Mabaraza ya Katiba. Mwishowe Tume imetakiwa kutengeneza Rasimu ya Katiba mpya itakayofikishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba kujadiliwa na Katiba mpya kutungwa. Mchakato wa Katiba utahitimishwa kwa wananchi kupiga kura ya maoni ya kuamua kama wanaikubali au kuikataa Katiba mpya.

Tarehe 6 Aprili, 2012 nilifanya uteuzi wa
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuwaapisha tarehe 13 Aprili, 2012.
Tume ilianza kazi tarehe 2 Mei, 2012 na kuikamilisha kwa mafanikio, hatua zote
zilizoihusu na kukabidhi kwangu na kwa Rais wa Zanzibar, Taarifa ya Tume na
Rasimu ya Katiba tarehe 30 Desemba, 2013. Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume,
Mheshimiwa Joseph Warioba kuwasilisha Rasimu hiyo mbele ya Bunge hili tukufu
tarehe 18 Machi, 2014, kinahitimisha rasmi kazi ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba. Kazi inayofuatia ni ya Bunge hili kujadili, kuamua na kutunga Katiba
mpya. Baada ya hapo Katiba mpya itafikishwa kwa wananchi kwa uamuzi wa mwisho
kwa njia ya kupiga kura ya NDIYO au HAPANA.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Rasimu ya Katiba ilichapishwa kwenye gazeti la Serikali na magazeti mengine yanayosomwa na wananchi kama ilivyoagizwa katika Kifungu cha 20(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Pamoja na hayo, Taarifa ya Tume na Rasimu ya Katiba viliwekwa wazi kwenye tovuti ya Tume kwa kila mtu kusoma. Inafurahisha kuona kuwa watu wengi wameisoma Taarifa ya Tume na Rasimu ya Katiba na kumekuwa na mjadala mpana kuhusu nyaraka zote hizo muhimu. Watu wengi wametoa maoni yao na wanaendelea kufanya hivyo. Kwa maoni yangu hili ni jambo jema sana na ni kielelezo thabiti kuwa demokrasia imestawi na inazidi kuota mizizi Tanzania. Pia, kwamba, Watanzania wako huru kushiriki na kutoa maoni yao kwa mambo yanayowahusu.
Pongezi kwa Tume

Kwa mara nyingine tena narudia kutoa pongezi za dhati kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uongozi wa Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba akisaidiwa na Mheshimiwa Jaji Augustino Ramadhani, kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya. Kazi yao haikuwa rahisi hasa ukizingatia ukubwa wa nchi yetu, wingi wa watu wake, utitiri wa taasisi na pigo la kumpoteza Mjumbe mwenzao muhimu Dkt. Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya haki katikati ya mchakato.

Pamoja na hayo, kwa bidii kubwa Wajumbe wa Tume
wameweza kutembelea mikoa yote nchini na kuwafikia watu 351,644 waliotoa maoni
yao kwa mdomo na kwa maandishi. Halikadhalika, walipokea na kuchambua maoni
772,211 kutoka kwa wananchi na taasisi mbalimbali. Baada ya kupokea maoni ya
wananchi, kufanya utafiti na kwa kutumia maarifa na uzoefu wao, Wajumbe
wakafanya kazi ngumu, kuliko yote, ya kutengeneza Rasimu ya Katiba iliyoko
mbele ya Bunge hili. Ni kweli kwamba Wajumbe hawakuweza kuwafikia wananchi wote
wa Tanzania, lakini wameweza kuwafikia wananchi wengi, ambao kwa kiasi kikubwa
wanawakilisha taswira na mitazamo mipana ya jamii yetu.
Baadhi ya Masuala Yaliyojitokeza Katika Mjadala wa
Mapendekezo ya Tume
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tume imefanya kazi nzuri, yenye thamani kubwa
na ya manufaa kwa taifa la Tanzania. Rasimu imeandikwa vizuri na kwa weledi wa
hali juu. Tume imetoa mapendekezo ambayo kwa kiasi kikubwa yanahuisha na
kuboresha Katiba ya nchi yetu, kwa namna ya pekee. Katiba inayopendekezwa,
imejumuisha dhana na mambo kadhaa mapya yanayokwenda vyema na wakati tulionao
na kuweka msingi mzuri kwa huko mbele tuendako. Kwa taratibu za kawaida za
marekebisho ya Katiba tuliyonayo, isingekuwa rahisi kuingiza mambo mengi mapya
kiasi hiki.
Wajumbe Wana Kazi Kubwa
Wajumbe Wana Kazi Kubwa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Waheshimiwa Wajumbe;
Rasimu ya Katiba ni kitabu kikubwa kilichosheheni mambo mengi. Kina kurasa 106, sura 17 na ibara 271. Wajumbe wa Bunge hili mnatakiwa kusoma na kuelewa vizuri kila kilichoandikwa ili muweze kufanya uamuzi ulio sahihi. Mnawajibika kuchambua kwa kina na umakini mkubwa kila kilichomo, sura kwa sura, ibara kwa ibara, sentensi kwa sentensi na hata neno kwa neno. Hamna budi kujiridhisha kuhusu uandishi wa vifungu vya Rasimu ya Katiba na kufaa kwa dhana mbalimbali zilizoingizwa na kujengeka katika Rasimu.

Kile ambacho Wajumbe mtaona kinastahili kuboreshwa au kurekebishwa au kufutwa msisite kufanya hivyo ili Watanzania wapate Katiba iliyo bora. Msipofanya hivyo kuna hatari ya kupata Katiba ambayo ni ngumu kuitekeleza. Aidha, tunaweza kuwa na Katiba ambayo itanung’unikiwa na watu wengi na kusababisha madai ya kutaka ifanyiwe marekebisho muda mfupi baada ya kupitishwa. Bunge hili linao wajibu maalum wa kuzuia balaa hilo lisitokee katika nchi yetu. Ngazi mbalimbali zilizowekwa katika mchakato huu ni kama chujio la kuepusha hali hiyo isitokee. Kile ambacho hakikuonekana katika hatua moja kitaonekana katika hatua inayofuata na kurekebishwa. Nawaomba fursa mliyonayo muitumie vizuri.

Nimekwishaeleza kuwa moja ya jambo mnalotegemewa kufanya ninyi wenzetu mliopewa dhamana ya kutunga Katiba ya nchi yetu ni kujiridhisha na uandishi wake. Yapo maoni yaliyotolewa kuhusu uandishi ambayo naomba myatafakari na kuamua ipasavyo. Kwa mfano, kuna baadhi ya vifungu vya Katiba vinayopendekezwa vimekuwa na mambo mengi mno kuliko inavyostahili Katiba kuwa (too prescriptive). Pia kuna mawazo kwamba baadhi ya mambo hayangetakiwa kuwa katika Katiba bali yawe kwenye Sheria zinazotafsiri utekelezaji wa Katiba yenyewe.

Yako mambo yaliyotajwa kwenye Katiba ambayo
yanatakiwa kuelezwa wazi kuwa mtu hatakwenda mahakamani kuidai Serikali impatie
(non justiciable). Mambo yaliyotajwa kwenye Katiba ni mazuri na yanavutia,
lakini lazima yaendane na uwezo wa nchi na uchumi wake kuhimili. Simaanishi
kwamba tuyatoe kwenye Katiba, bali yabakie kama dhamira pale uwezo wa nchi
utakaporuhusu yatekelezwe. Tusipofanya hivyo, kuna hatari ya Serikali kujikuta
inalaumiwa au hata kufikishwa mahakamani kila wakati kwa madai ya jambo moja au
jingine ambayo haina uwezo nayo. Ni muhimu sana mambo kama hayo muyatazame ili
tusije kuwa na Katiba ambayo ni ngumu kutekeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Yapo pia maoni kuwa baadhi ya vifungu vina upungufu katika uandishi wake, hivyo kuhitaji kufanyiwa marekebisho. Isipofanyika hivyo kunaweza kuwepo athari na nyingine zinaweza kuwa mbaya. Kwa mfano, Ibara ya 2 ya Rasimu inayotambulisha eneo na mipaka ya nchi yetu. Ibara hiyo inasomeka kuwa “Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanganyika likijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar likijumuisha sehemu yake ya bahari”.

Maelezo hayo yameacha kutambua, kwa upande wa
Tanzania Bara, sehemu yetu ya maziwa na mito ambayo ni kubwa sana. Kwa nini
tuache kuitaja? Je hatutoi nafasi kwa nchi tunazopakana nazo siku moja wakaja
kupora sehemu zetu hizo na sisi kukosa utetezi kwa kuwa hata Katiba yetu
haikuyatambua maeneo hayo kuwa ni yetu? Hili ni jambo kubwa ambalo Bunge hili
lazima mlirekebishe. Wakati ndiyo huu hakuna mwingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo jingine kuhusu uandishi ni mgongano kati ya pendekezo la msingi la Tume la kuwa na muundo wa Serikali tatu na majukumu ya Serikali ya Muungano ambayo kimsingi ni majukumu ya Serikali za nchi washirika. Katika Rasimu hii malengo ya taifa yameainishwa na Serikali ya Muungano inatakiwa kuhakikisha kuwa malengo hayo yanatekelezwa na itoe taarifa Bungeni. Katika mfumo wa Serikali tatu unaopendekezwa na Tume masuala yahusuyo uchumi na maendeleo ya jamii kama vile kukuza kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara, pembejeo, elimu, hifadhi ya jamii na kadhalika yako chini ya mamlaka ya Serikali za nchi washirika. Mamlaka ya Serikali ya Muungano ni kwa mambo saba tu yafuatayo:- Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano, Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano, Uraia na Uhamiaji, Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya Nje, Usajili wa Vyama vya Siasa, Ushuru wa Bidhaa na Mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.

Kwa Rasimu kupendekeza muundo wa Serikali tatu
na kuipa Serikali ya Muungano majukumu ambayo haina mamlaka nayo, ni kuzusha
utata na migongano kati ya Serikali ya Muungano na nchi washirika. Mkichagua
mfumo wa Serikali tatu, inawalazimu muyaondoe mambo hayo kwani Serikali ya
Muungano haistahili kuyatekeleza na wala haina uwezo wa kuweka masharti kwa
Serikali za nchi washirika kwa mambo yaliyo kwenye mamlaka ya nchi hizo. Lakini
kama mtaamua tuendelee na muundo wa Serikali mbili, mambo haya mazuri
yanatekelezeka na Serikali ya Muungano bila ya matatizo. Katika uandishi wa
Rasimu Utumishi katika Serikali ya Muungano haumo katika Orodha ya Mambo ya
Muungano. Ni lazima liwemo. Hayo ni baadhi tu ya masuala yahusuyo uandishi
katika Rasimu. Naamini mkiisoma Rasimu kwa makini mnaweza kuyagundua mengineyo.
Dhana Mpya
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Katika Rasimu kuna dhana mpya na mambo mapya kadhaa yaliyoingizwa ambayo yanabadili utaratibu wa sasa wa uendeshaji wa nchi na mambo mbalimbali. Nawaomba mfanye uchambuzi wa kina kwa kila kinachopendekezwa na kujiridhisha kuhusu kufaa kwake na manufaa yake. Fanyeni hivyo ili tujihakikishie kuwepo kwa mambo mazuri na uendeshaji mzuri wa shughuli katika taifa letu changa.

Mambo ni mengi na kwa ufinyu wa muda sitaweza
kuyazungumzia yote. Niruhusuni nizungumzie baadhi ya dhana na mambo mapya
yaliyomo katika Rasimu. Jambo la kwanza, kwa mfano, linahusu Ibara ya 128
(2)(d) inayoleta dhana ya “Mbunge kupoteza Ubunge iwapo atashindwa kufanya kazi
za Mbunge kwa miezi sita mfululizo kutokana na maradhi au kizuizi ndani ya
gereza”.
Watu hawana tatizo na Mbunge kuwa kizuizini
ndani ya gereza kama amepatikana na hatia Mahakamani na kuhukumiwa kifungo.
Lakini, isijekuwa yuko rumande kwa tuhuma akisubiri kesi kusikilizwa. Je akija
kuonekana hana hatia na kuachiliwa? Naungana na wale wanaoshauri kuwa jambo
hili lifafanuliwe vizuri na kutambua Mbunge kutiwa hatiani na kupata adhabu ya
kifungo cha kipindi hicho. Ni bora ifanyike hivyo sasa ili kuondoa
mikanganyiko. Hakuna haja ya kusubiri mpaka jambo hili lije kufafanuliwa
baadaye kwa Sheria itakayotungwa na Bunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa upande wa mtu kupoteza Ubunge kwa sababu ya “kuugua kwa miezi sita mfululizo” ni maoni ya watu wengi kuwa huu ni ukatili ambao haustahili kufanywa na Katiba. Kuugua ndiyo ubinadamu na wakati mwingine Mbunge anaweza kupata ajali akiwatumikia wananchi wa Jimbo lake. Anaweza kuugua kwa miezi sita au zaidi na kupona kabla ya kipindi chake cha Ubunge kufika mwisho. Kwa nini awekewe ukomo wa miezi sita? Katiba ya mwaka 1977 tunayotumia sasa haina sharti hilo. Watu wanauliza hoja na haja ya kuwa na sharti hili kwenye Katiba mpya ni ipi? Wanasema kwa kweli anachostahili Mbunge huyu kufanyiwa ni kuuguzwa afya yake iimarike ili aendelee kutumikia watu wake, na siyo kupoteza uongozi wake. Tusiwatie watu kishawishi cha kukatiza matibabu ili kukwepa sharti hilo. Ni vyema jambo hili mkalitazama kwa makini, na muone kama linastahili kuwepo au hapana.

Katika Rasimu hii imeingizwa dhana mpya ya kuweka ukomo wa vipindi vitatu kwa Wabunge. Tena mapendekezo haya hayasemi vipindi vitatu mfululizo au la!. Jambo hilo limezua mjadala motomoto katika jamii. Ni vizuri mkajiridhisha juu ya sababu za msingi na manufaa ya kufanya hivyo hapa Tanzania. Mazoea yetu na ya kwingineko duniani ni kuweka ukomo kwa Wakuu wa Nchi kwa sababu nzuri na rahisi kuzielezea. Lakini, kuwawekea ukomo Wabunge ni jambo jipya na huenda Tanzania tukawa wa kwanza. Nashawishika kuungana na wale wanaopendekeza kuwa pengine ni mapema mno kuanzisha utaratibu huo hapa kwetu.

Nachelea kuwa tutainyima nchi yetu fursa ya
kupata watu wenye maarifa na uzoefu mzuri wa uongozi kwa nafasi ya Ubunge au
kwa nafasi za uongozi wa Taifa bila ya sababu za msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo lingine jipya linalopendekezwa na Tume ni utaratibu wa kumuondoa Mbunge katikati ya kipindi chake cha uongozi. Kwa hoja linaonekana kuwa jambo jema lakini naomba athari zake mzitafakari vizuri. Kuna hatari ya kuanzisha misuguano kwenye Majimbo na kuwaacha Wabunge wasifanye kazi zao kwa utulivu bali wawe wanajihami dhidi ya wapinzani wao kuwatengenezea fitna za kuwatoa. Utaratibu unaopendekezwa wa Chama chake kujaza nafasi ya Mbunge inapokuwa wazi katika mazingira hayo nao unaweza kuwa ndicho kichocheo kikubwa cha vuguvugu la kumuondoa Mbunge. Walioshindwa kwenye kura ya maoni wanaweza kufanya kazi ya kuwachimba wenzao mpaka waondoke. Jipeni muda wa kupima faida na hasa thamani inayoongezwa na kuanzisha utaratibu huo. Naomba tujiridhishe kama jambo hili jipya lina tija. Hivi kupewa nafasi kila miaka mitano kurudi kwa wananchi hakutoshi kumuondoa Mbunge ambaye watu wamemchoka?

Muundo wa Muungano
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo lingine kubwa lililopendekezwa na Tume ambalo limevuta hisia za karibu watu wote nchini linahusu muundo wa Muungano wetu kuwa wa Serikali tatu badala ya mbili za sasa. Pendekezo hili limezua mjadala mkubwa tangu lilipotolewa katika Rasimu ya kwanza na kurudiwa katika Rasimu ya pili. Wakati mwingine mjadala umekuwa mkali na wa hisia kali kwa kila upande.

Kwa kweli hili ndilo jambo kubwa kuliko yote
katika Rasimu kwa sababu linapendekeza kuanzishwa kwa muundo na mfumo mpya wa
kuendesha nchi yetu. Hii ndiyo agenda mama ya Bunge hili ambayo kila Mtanzania
anasubiri kwa hamu uamuzi wenu utakuwa upi. Ombi langu kwenu ni kuwa watulivu
mnapojadili suala hili. Epukeni jazba ili mfanye uamuzi ulio sahihi. Lazima
mtambue uamuzi usiokuwa sahihi kwa jambo hili una hasara kubwa. Tunaweza
kupoteza kitu tulichokijenga kwa gharama kubwa kwa nusu karne iliyopita.
Tanzania inaweza kuwa nchi iliyojaa migogoro na matatizo mengi ambayo hatunayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wajumbe;
Kama alivyoeleza Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba, mara kadhaa, mjadala au madai ya kutaka muundo wa Serikali tatu si jambo jipya. Ulikuwepo hata wakati wa mazungumzo ya kuunganisha nchi zetu mbili mwaka 1964. Ulikuwa kiini cha kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar mwaka 1984. Muundo huu uliwahi kupendekezwa na Tume ya Nyalali mwaka 1992, ndiyo hoja ya G55 mwaka 1993 na umependekezwa pia na Tume ya Jaji Kisanga ya mwaka 1998. Lakini mara zote hizo mapendekezo hayo hayakukubaliwa.

Waasisi wa taifa letu, yaani Mwalimu Julius
Nyerere, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika wakati ule na Sheikh Abeid
Amani Karume, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar wakati ule,
waliamua kuchagua Muungano wa Serikali mbili tulionao sasa. Walitoa sababu
mbili kuu: “ni muundo unaoihakikishia Zanzibar kuwa haimezwi na Tanganyika; na
pia unaiepusha Tanganyika kubeba mzigo mkubwa wa kugharamia Serikali ya
Tanganyika na ile ya Muungano”.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Natambua kuwepo kwa rai ya kutaka Mwalimu Nyerere asitumiwe katika mjadala huu. Nionavyo mimi ni vigumu kuacha kujadili fikra za Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume katika jambo hili. Wao ndiyo wa mwanzo kujadili na kukubaliana kuwa mfumo wa Serikali mbili ndiyo bora kwa nchi yetu. Iweje leo tunapozungumzia kuubadili, mawazo yao yawe hayafai kutumika au hata kuzungumzwa. Hivi hasa mawazo ya nani pekee ndiyo bora zaidi kutumika? Tutakuwa hatuutendei haki mjadala huu na sisi wenyewe tunaoshiriki katika mchakato huu. Rai yangu kwenu ni kuwa mzitazame hoja zote kwa marefu na mapana yake ili mpime kama zipo sababu za kuubadili muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili na kuleta wa Serikali tatu. Na, kama zipo mabadiliko hayo yaweje! Lazima mfanye uamuzi kwa utambuzi na hoja zenye mashiko. (you must make an informed decision).

Tume imetoa sababu mbili kubwa za kupendekeza muundo wa Serikali tatu. Sababu ya kwanza ni kwamba ndiyo matakwa ya Watanzania wengi kote Zanzibar na Tanzania Bara. Inaeleza kuwa idadi kubwa ya Watanzania waliotoa maoni, yaani asilimia 60.2 wa kutoka Zanzibar wanaunga mkono muundo wa Serikali ya Mkataba, na asilimia 61.3 wa kutoka Tanzania Bara wanaunga mkono muundo wa Serikali tatu. Sababu ya pili ni kwamba muundo huo unatoa majawabu ya uhakika na endelevu kwa changamoto za muundo wa sasa wa Serikali mbili zinazonung’unikiwa na watu wa pande zetu mbili za Muungano.

Sababu hizi mbili kuu zilizotolewa na Tume zimezua mjadala mkali katika jamii. Wapo wanaokubaliana na Tume na wapo wasiokubaliana nayo. Wapo wanaosema Tume imesema kweli kwamba Watanzania wengi wanaunga mkono muundo wa Serikali tatu, hivyo muundo wa Serikali tatu hauepukiki. Ndiyo matakwa ya wengi hivyo msemo wa Kiswahili usemao wengi wape uheshimiwe.

Lakini wapo wanaodai kuwa takwimu za Tume hazionyeshi ukweli huo.
Wanasema kuwa taarifa ya Tume imeonesha kuwa Watanzania waliotoa maoni yao kwa
Tume kwa mdomo na maandishi walikuwa 351,664. Kati yao ni wananchi 47,820 au
sawa na asilimia 13.6 ndiyo waliokerwa na muundo wa Muungano hivyo
wakauzungumzia. Wananchi 303,844 au sawa na asilimia 86.4 muundo wa Muungano
kwao halikuwa tatizo, ndiyo maana hawakuuzungumzia kabisa. Wanahoji kuwa iweje
leo asilimia 13.6 ya Watanzania wote waliotoa maoni wageuke kuwa ndiyo
Watanzania walio wengi!
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Wanasema pia, kwamba mbona Taarifa ya Tume yenyewe, kuhusu takwimu (uk. 66 na 67), inaonesha kwamba kati ya hao watu 47,820 waliotoa maoni kuhusu Muungano, ni watu 17,280 tu ambao ni sawa na asilimia 37.2 ndiyo waliotaka muundo wa Serikali tatu, asilimia 29.8 walitaka Serikali mbili, asilimia 25.3 walipendekeza Serikali ya Mkataba na asilimia 7.7 walipendekeza Serikali moja. Hii hoja ya Watanzania wengi kutaka Serikali tatu msingi wake upi?

Takwimu za Tume (uk. 57) zinaonyesha, vilevile kuwa Tume ilipokea maoni 772,211. Kati ya hayo asilimia 10.4 tu ndiyo yaliyozungumzia muundo wa Muungano na asilimia 88.6 hayakuzungumzia Muungano bali mambo mengine. Hivyo basi wanahoji pia kwamba kama muundo wa Muungano ungekuwa ni jambo linalowakera Watanzania wengi, lingedhihirika kwenye idadi ya watu waliotoa maoni na kwenye idadi ya maoni yaliyotolewa. Yote hayo hayakujitokeza. Waliouzungumzia Muungano walikuwa asilimia 13.6 tu ya watu wote waliotoa maoni na maoni yanayohusu Muungano yalikuwa asilimia 10.4 ya maoni yote. Hivyo basi, wanauliza “usahihi wa hoja ya Watanzania wengi kutaka Serikali tatu uko wapi?”

Changamoto za Muundo wa Serikali Mbili
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe;
Kama nilivyokwishagusia awali, sababu ya pili ambayo Tume inatoa kuhusu kufaa kwa muundo wa Serikali tatu ni kwamba mfumo huu unajibu changamoto nyingi za muundo wa Serikali mbili. Tume imeainisha vizuri changamoto za muundo wa Serikali mbili. Kwa upande wa Zanzibar wanalalamikia kile kinachoitwa Tanzania Bara kuvaa koti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kutumia mamlaka ya Serikali ya Muungano kujinufaisha yenyewe. Fursa hiyo Zanzibar hainayo. Aidha, wanasema mipaka na mamlaka ya Serikali ya Muungano kwa mambo ya Muungano, na kwa mambo ya Tanzania Bara haijaainishwa vizuri ikaeleweka. Wazanzibari pia, wanazungumzia mkanganyiko kuhusu ugawanaji wa mapato, na jinsi ya kuchangia shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vilevile, wanalalamikia Rais wa Zanzibar kuondolewa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Aidha, kuna malalamiko kuwa orodha ya mambo ya Muungano iliyoongezwa
kutoka mambo 11 mwaka 1964 mpaka 22 mwaka 1992 imepunguza uhuru wa Zanzibar kwa
mambo yake ya ndani.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa upande wa Tanzania Bara, Tume inaeleza kuwepo kwa manung’uniko kuwa Muungano wa Serikali mbili umepoteza utambulisho wa kihistoria wa Tanganyika na fursa ya watu wa upande wa Tanzania Bara kutetea maslahi yao ndani ya Muungano. Wanasema Zanzibar sasa imekuwa nchi huru; ina bendera yake, wimbo wake wa taifa na Serikali yake. Aidha, wanasema Zanzibar imebadili Katiba na kujitambulisha kama nchi na kuchukua madaraka ya Bunge la Muungano, kwa vile Sheria zinazotungwa na Bunge lazima zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi kupata kibali cha kutumika Zanzibar. Wananchi wa Tanzania Bara pia wanalalamikia kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wa kutoka Zanzibar wanayo haki hiyo Tanzania Bara. Na wao vilevile wananung’unikia mkanganyiko kuhusu ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Hizi ndizo baadhi ya changamoto ambazo Tume inaona jawabu lake ili kuzitanzua ni kubadili muundo wa Muungano kuwa wa Serikali tatu badala ya mbili za sasa.

Faida za Muundo wa Serikali Tatu
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imefafanua kwamba mfumo wa Serikali tatu utagawanya vizuri madaraka kati ya mamlaka tatu za Muungano. Unawezesha Washirika wa Muungano kubaki na utambulisho wao wa kihistoria na kiutamaduni na hivyo, utawezesha kuondoa hisia za Zanzibar kumezwa na Muungano. Pia unawezesha kila upande wa Tanzania kuendesha mambo yake yasiyo ya Muungano kadri wanavyoona inafaa. Vile vile unaweza ukaleta ushindani wa kimaendeleo baina ya washirika na hivyo kusaidia kukuza maendeleo ya nchi.

Faida za Muundo wa Serikali Mbili
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Pamoja na kuainisha changamoto za muundo wa Serikali mbili na kupendekeza kuwa muundo wa Serikali tatu ndio utakaosaidia kuzitatua, Tume haikuacha kutambua manufaa na mchango muhimu uliotolewa na muundo wa Serikali mbili kwa nchi yetu. Tume inasema kuwa muundo wa Serikali mbili unapunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za umma. Umesaidia kujenga uhusiano na ushirikiano mzuri katika nyanja mbalimbali baina ya wananchi wa pande zetu mbili za Muungano. Umezuia mkubwa kummeza mdogo; na umedumisha Muungano mpaka kuufikisha hapa ulipo tangu kuasisiwa kwake takriban miaka 50 iliyopita (1964). Aidha, umesaidia kudumisha amani, umoja na utulivu hapa nchini.

Changamoto za Muundo wa Serikali Tatu
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Pamoja na kuelezea ubora wa muundo wa Serikali tatu kama jawabu kwa changamoto za Serikali mbili, Tume inakiri kuwa hata muundo huu nao una changamoto zake. Kwanza kabisa, Taarifa ya Tume inaeleza kuwa kutakuwa na gharama kubwa za uendeshaji wa shughuli za umma. Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba alitutoa hofu kuhusu gharama ingawaje mwaka 1993, Mwalimu alikuwa na mawazo tofauti. Alisema kwamba: “watu …wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yo yote kati ya hizo ingekuwa ndogo, (Waulizeni Wazanzibari) na wala gharama ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo hata bila gharama ya mambo yasiyo ya Shirikisho”. Ni matumaini yangu kwamba katika mjadala wenu mtajipa nafasi ya kulitafakari suala hili kubwa na nyeti.

Tume imesema pia kwamba, Muundo huu, unaweza kuibua tatizo la uchangiaji
wa gharama za uendeshaji wa shughuli za umma baina ya nchi washirika. Vilevile,
kuna uwezekano wa kuwepo sera zinazokinzana au kutofautiana juu ya masuala ya
msingi ya nchi na kuzua mgogoro kati ya washirika wa Muungano na baina ya nchi
washirika na Serikali ya Muungano. Aidha, upo uwezekano mkubwa kwa muundo huu
kuleta tofauti za kimaendeleo baina ya pande mbili za Muungano kutokana na kila
upande kuwa na sera na mipango tofauti.
Tume pia imeelezea hatari ya muundo wa Serikali tatu kukuza hisia za
utaifa (nationalistic feelings) kwa nchi washirika, hivyo kuweza kudhoofisha
Muungano. Muundo huu pia unaweza kuleta misuguano (paralysis and deadklocs in
decision making) katika kufanya uamuzi juu ya masuala muhimu ya kitaifa.
Changamoto hizo si tu zinaweza kuwa tishio kwa ustawi wa Muungano bali pia hata
uhai wake. Kwa ajili hiyo kuchagua muundo wa Serikali tatu kuna maana ya
kufanya kazi ya ziada ya kuzikabili changamoto hizi ili zisiue Muungano
wenyewe. Changamoto ambazo si ndogo hata kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Wanaounga mkono muundo wa Serikali mbili wanasema kuwa kwa mlolongo huu wa changamoto zilizoainishwa na Tume yenyewe, unadhihirisha kuwa muundo wa Serikali tatu hautapunguza matatizo ya Muungano wetu bali utayaongeza maradufu kuliko ilivyo sasa. Wanakiri kuwepo kwa changamoto katika muundo wa sasa wa Muungano. Hata hivyo, wanaamini zinaweza kushugulikiwa na kupatiwa ufumbuzi bila ya kuhitaji kuwa na Serikali ya tatu. Wanatoa mifano kadhaa ya jinsi Serikali zetu zilivyoshughulikia changamoto za Muungano katika kipindi cha uhai wake na mafanikio yaliyopatikana.
Katika kushughulikia kero za Muungano, Serikali zetu mbili ziliunda Tume ya Shelukindo mwaka 1992 na Kamati ya Pamoja ya Serikali zetu mbili mwaka 1993. Mambo mengi yaliyoainishwa katika Tume ya Shelukindo na Kamati ya Pamoja yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Kwa upande wa kero zilizoelezwa kwenye Tume ya Shelukindo, ilipofikia mwaka 2006 yalikuwa yamebakia mambo 13 kati ya 31. Kwa jumla, kwa kero zilizoibuliwa na Tume ya Shelukindo na Kamati ya Pamoja, hivi sasa yamesalia mambo sita tu. Kimsingi ni mambo yahusuyo maslahi ya kiuchumi na yote yapo katika hatua nzuri za kuyamaliza. Mambo hayo ni:

1. Mgawanyo wa mapato:
(a) Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki
(b) Mgawanyo wa Mapato yatokanayo na faida ya Benki Kuu.

2. Utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asili.
3. Ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za nje.
4. Ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za Muungano.
5. Usajili wa vyombo vya moto.
6. Tume ya Pamoja ya Fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Serikali zetu mbili zimeamua kwa dhati kutumia fursa ya mchakato huu wa mabadiliko ya Katiba kuyamaliza yale yanayohitaji kuingizwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mambo hayo ni matatu yafuatayo:

1. Utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asili.
2. Ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za nje.
3. Tume ya Pamoja ya Fedha.
Matatu mengine yatamalizwa kwa kutumia taratibu za kiutawala. Hali kadhalika, katika kipindi cha mpito kinachopendekezwa na Tume yaani 2015 – 2018 ni nafasi nzuri ya kushughulikia masuala yenye migongano kati ya Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano. Mimi naishi kwa matumaini na kwa vile tunayo dhamira njema ya kuimarisha Muungano wetu, naamini tutaweza kuziondoa tofauti zilizopo.

Orodha ya Mambo ya Muungano
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kuhusu orodha ya mambo ya Muungano kuwa 22 badala ya 11 ya awali, napenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hazina kigugumizi wala upungufu wa dhamira ya kisiasa ya kuyapunguza yale yanayopunguzika. Napenda kwanza kabisa, ieleweke kuwa kilichoongeza orodha hiyo si hila za Serikali ya Muungano kutaka kupunguza madaraka ya Zanzibar kwa mambo yake ya ndani. Na, wala siyo udhaifu wa viongozi wa Zanzibar katika kutetea maslahi ya nchi yao. La hasha.
Pili, naomba ieleweke kuwa, kila kilichoongezwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano kilikuwa na sababu inayoeleweka, inayoelezeka na iliyokubalika na pande zote mbili za Muungano. Hakuna hata jambo moja lililoingizwa kwenye Katiba kwa kificho. Taratibu stahiki za kikatiba na kisheria zilifuatwa. Hoja ziliwasilishwa Bungeni na kujadiliwa kwa uwazi na uamuzi ulifanywa na Bunge kwa kuzingatia kanuni ya theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano. Kumbukumbu zipo katika Hansard za Bunge la Muungano, ambazo ziko wazi kwa kila mtu anayetaka kuzisoma asome. Nashauri mkazisome ili mpate kujua ukweli na undani wa kila kilichoongezwa na sababu za kufanya hivyo.

Nchi zetu mbili zilipoungana mwaka 1964 na kuzaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kulikuwa na mambo 11 kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano,
2. Mambo ya Nje,
3. Ulinzi,
4. Polisi,
5. Hali ya Hatari,
6. Uraia,
7. Uhamiaji,
8. Biashara ya nje na mikopo,
9. Utumishi katika Serikali ya Muungano,
10. Kodi ya Mapato, Kodi ya Makampuni, Ushuru
wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa,
11. Bandari, Mambo ya Anga, Posta na Simu.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kati ya mwaka 1965 na 1992 mambo ya Muungano yaliongezeka kutoka 11 hadi kufikia 22, kimsingi kutokana na mambo mbalimbali yaliyotokea nchini na kwenye ukanda wetu wa Afrika Mashariki. Pande zetu mbili za Muungano zilikubaliana kuwa mambo hayo yaongezwe katika Katiba na taratibu za kisheria na Kikatiba zilifuatwa. Kwa idhini yako naomba nitoe maelezo kwa ufupi kwa yale yaliyoongezwa na kitu kilichosababisha mabadiliko hayo kufanywa.

1. Jambo la kwanza kuongezwa, yaani la 12
lilikuwa ni “sarafu, mabenki na fedha za kigeni”. Hii ilifanyika tarehe 10
Juni, 1965 kufuatia kuvunjika kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (East
African Currency Board) mwaka 1964. Kwa ajili hiyo, kila nchi mwanachama wa
Jumuiya ililazimika kuwa na sarafu yake na mipango yake ya kusimamia mambo yake
ya kibenki na fedha. Serikali zetu mbili zilikubaliana masuala hayo
yashughulikiwe na Serikali ya Muungano na Muswada husika wa Bunge uliidhinishwa
kuwa Sheria na Mzee Abeid Amani Karume aliyekuwa akikaimu Urais tarehe 10 Juni,
1965.
2. Tarehe 11 Agosti, 1967 yaliongezwa mambo yafuatayo kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano:-
(a) Leseni za Viwanda na Takwimu, (Jambo la 13)
(b) Elimu ya Juu, (Jambo la 14)
(c) Jambo la 15 lilikuwa ni mambo yote yaliyokuwa kwenye Nyongeza ya 10 ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nyongeza hiyo ilikuwa na mambo 27 ambayo Serikali ya Muungano ilipewa jukumu la uratibu. Mambo hayo ni pamoja na Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki, Utabiri wa Hali ya Hewa, Utafiti, Vipimo na Mizani, Huduma ya Usafiri wa Reli, Barabara, Usafiri wa Majini na kadhalika.
3. Tarehe 22 Julai, 1968 “rasilimali ya mafuta, petroli na gesi asilia” iliongezwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano na kuwa jambo la 16. Kimsingi Serikali ya Muungano ilipewa jukumu la kuagiza mafuta ya petroli na gesi asilia kwa ajili ya nchi nzima. Baada ya kupanga upya Orodha ya Mambo ya Muungano, suala la rasilimali ya mafuta likawa la 15.
4. Tarehe 22 Novemba, 1973 Baraza la Mitihani la Taifa liliongezwa na kuwa jambo la 16. Hii ilifuatia kuvunjika kwa Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki mwaka 1971 na hivyo nchi yetu kulazimika kuunda Baraza la Mitihani la Taifa mwaka 1973.
5. Mwaka 1984 yalipofanyika mabadiliko makubwa katika Katiba ya mwaka 1977, Orodha ya Mambo ya Muungano ilipangwa upya. Mambo yaliyokuwemo kwenye Nyongeza ya 10 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuorodheshwa kama Jambo la 15 katika Orodha ya Mambo ya Muungano yalipunguzwa na kubaki matano. Mambo hayo yalipewa namba kama ifatavyo:- Usafirishaji wa Anga kuwa Jambo la 17, Utafiti kuwa la 18, Utabiri wa Hali ya Hewa kuwa la 19 na Takwimu kuwa la 20 na Mahakama ya Rufani ya Tanzania ikawa jambo la 21.
6. Tarehe 17 Mei, 1992 likaongezwa jambo la “Uandikishaji wa Vyama vya Siasa” na kuwa jambo la 22. Hii ilifuatia kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa na hasa uamuzi kuwa vyama vitakuwa vya kitaifa.

Bila ya shaka maelezo haya yatasaidia kuelezea nini kimeongezwa na mazingira ya kuongezwa kwake ni yepi. Kulikuwepo na sababu za msingi na wala siyo hila ya namna yo yote ile iliyofanywa na mtu ye yote mwenye nia mbaya na Zanzibar. Kama tulivyoona mambo mengi yalihusu kilichokuwa kinatokea ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kila yalipotokea mabadiliko katika uendeshaji wa shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki, huduma zilizokuwa zikitolewa na Jumuiya zilikabidhiwa Serikali ya Muungano kubeba kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kiuchumi. Yale yaliyokuwa yanagusa sehemu zetu mbili za Muungano yaliingizwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano. Mengineyo yaliachiwa kila upande kushughulikia ilivyoona inafaa. Kwa maana hii basi, mambo ambayo yalitokana na uamuzi wetu wenyewe ni mawili tu. Mambo hayo ni rasimali ya mafuta na gesi asilia (1968), na uandikishaji wa vyama vya siasa (1992).

Ni msimamo wa Serikali zetu mbili, tangu mwanzo mpaka leo kwamba, iwapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshajenga uwezo wake wa kufanya baadhi ya mambo katika Orodha ya Mambo ya Muungano ipewe uhuru wa kufanya hivyo. Lililo muhimu ni kuwa zisiondolewe tunu zenyewe za Muungano wetu. Ndiyo maana, mambo kama vile bandari, takwimu, kodi ya mapato, leseni za biashara, utafiti na mengineyo, yanasimamiwa na kuendeshwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuwemo kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano. Imekuwa hivyo kwa miaka kadhaa sasa na imethibitika kuwa Zanzibar inayamudu. Ni makusudio yetu kutumia fursa ya mchakato huu sasa kuyaondoa rasmi mambo hayo na mengineyo tutakayokubaliana kutoka kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.

Rasilimali ya Mafuta na Gesi Asilia
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kwa ajili hiyo tumekubaliana kuliondoa suala la rasilimali ya mafuta na gesi asilia lisiwe jambo la Muungano. Jambo hili tulishakubaliana tangu wakati wa Rais Amani Abeid Karume tuliondoe na hata alipokuja Rais Shein msimamo haukubadilika. Kilichotuchelewesha kutekeleza ni kuibuka kwa fikra za kuwa na mchakato huu wa Katiba mpya. Tuliona kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria wa kuondoa jambo hili katikati ya mchakato huu, ingeweza kuzua matatizo yasiyokuwa ya lazima. Tungeulizwa haraka ni ya nini tungeweza kukosa majibu.

Hatimaye wakati wake wa kulimaliza suala hili
sasa umefika. Misemo ya wahenga ya “subira yavuta heri” na “kawia ufike”
imetuongoza vyema tumefika mahali tunaweza kufanya hivyo. Zipo sababu mbili
zilizotushawishi kuamua kuitoa rasilimali hii kwenye Orodha ya Mambo ya
Muungano. Kwanza kwamba, siku hizi Serikali haiagizi mafuta. Kazi hiyo hufanywa
na makampuni binafsi. Pili, kwamba, rasilimali ya mafuta na gesi yakipatikana
Zanzibar ni suala la kiuchumi ambalo lipo kwenye mamlaka ya Zanzibar kama
ilivyo karafuu, hiliki, mwani na kadhalika. Au kama ilivyo dhahabu, gesi,
pamba, kahawa na kadhalika kwa upande wa Tanzania Bara. Hivyo, Zanzibar iachwe
kumiliki rasilimali yake ya kiuchumi.
Zanzibar na Ushirikiano wa Kimataifa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Jambo lingine muhimu ambalo Serikali zetu mbili zimelizungumza na kukubaliana tulitafutie ufumbuzi ni kuhusu Zanzibar kupata fursa ya kujiunga na mashirika ya kimataifa, kukopa na kupata misaada kutoka nchi za nje bila kizuizi. Kwa sasa fursa hiyo ina vikwazo vya namna mbalimbali. Ni ukweli usiopingika kuwa jambo hili limechangia kwa kiasi kikubwa kujenga hisia hasi kuhusu Muungano kwa upande wa Zanzibar. Aidha, limechangia sana kuchafua hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar kwa nyakati mbalimbali. Hata zile kauli kwamba Tanzania Bara imejificha kwenye koti la Serikali ya Muungano, na kutaka itoke ionekane ili iache kunufaika isivyostahili, zinazochangiwa sana na mazingira haya iliyonayo Zanzibar. Serikali zetu mbili zinaamini kuwa mambo haya yakipatiwa ufumbuzi tutakuwa tumeondoa kizingiti kikubwa katika ustawi wa Muungano wetu.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tumekubaliana kuwa, tutumie fursa za mchakato huu kuyamaliza mambo haya yaishe! Bahati nzuri dhana iliyopo katika Ibara ya 65(2) ya Rasimu inatoa jawabu mwafaka kwa tatizo hili. Tukikubaliana, itaipa Zanzibar “uwezo na uhuru wa kuanzisha uhusiano na ushirikiano na jumuiya au taasisi yo yote ya kikanda na kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi” bila kizuizi. Ni maoni ya Serikali zetu mbili kuwa fursa hiyo inaweza kutolewa kwa Zanzibar bila ya kulazimika kuwa na muundo wa Serikali tatu. Hatuuoni ulazima huo.

Kwa maoni yangu kitu kingine muhimu cha kufanya ni kuongeza msukumo, utakaohakikisha kuwa Tume ya Pamoja ya Fedha inatimiza ipasavyo majukumu yake. Wanaohusika na utekelezaji wa maamuzi yake wabanwe ipasavyo kutimiza wajibu wao. Iwekwe mifumo na masharti katika sheria au Katiba ya kuwabana watekelezaji kwa ajili hiyo. Hali kadhalika ihakikishwe kuwa, Akaunti ya Pamoja inaanzishwa bila ajizi na kutumika na pande zote. Aidha, mfumo wa mawasiliano na ushirikiano baina ya Serikali zetu mbili yaani Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, upewe nguvu ya kisheria na kama hapana budi upewe nguvu ya Kikatiba. Tukifanya hivyo tutafanikiwa kuyaweka mambo yote sawa hata bila ya kuhitaji kuunda Serikali ya tatu.

Katika mjadala kuhusu mapendekezo ya kuwa na muundo wa Muungano wenye Serikali tatu, wananchi wametoa maoni na mapendekezo mengi mazuri kuhusu changamoto za Serikali tatu zilizoainishwa na Tume na namna ya kuzitatua. Tena yapo maoni ya watu wanaopenda muundo wa Serikali tatu na wasiopenda muundo wa Serikali tatu. Nawaomba myatafakari kwa uzito unaostahili. Yapo mambo muhimu ya kuyatafutia ufumbuzi.

Kwanza, kwa mfano ni ile hoja kwamba
Serikali ya Muungano inayopendekezwa haikujengeka kwenye msingi imara. Haina
nguvu yake yenyewe za kusimama. Inategemea mno ihsani ya nchi washirika. Kwa
sababu hiyo inaweza kuanguka wakati wowote, na Muungano kusambaratika, iwapo
itakosa ihsani ya nchi washirika. Tena inaweza kuwa hivyo hata kama ni mmoja wa
washirika amefanya hivyo.
Pili, kwamba, haielekei Serikali hiyo ina chanzo
cha uhakika cha mapato ya kuiwezesha kusimama yenyewe na kutekeleza majukumu
yake. Ushuru wa bidhaa unaopendekezwa unatiliwa shaka kuwa hautatosheleza
mahitaji. Pia, kwamba, hakuna uhakika wa fedha hizo kupatikana kwa vile,
Serikali ya Muungano haina chombo chake chenyewe cha kukusanya mapato hayo.
Itategemea vyombo vya nchi washirika kuikusanyia na kuipelekea. Kuna hatari ya
shughuli za Serikali ya Muungano kusimama wakati wo wote au hata kusimama
kabisa kwa sababu ya nchi washirika kuchelewa au kushindwa kuwasilisha
makusanyo ya kutoka kwao.
Bahati mbaya Serikali ya Muungano haina uwezo
wala nyenzo za kuhakikisha kuwa mapato yake yanawasilishwa. Serikali hiyo haina
mamlaka ya kuzibana nchi washirika kuwasilisha au kuziwajibisha zisipofanya
hivyo. Katika mazingira hayo ni rahisi kwa Serikali ya Muungano kukwama na
kushindwa kutekeleza majukumu yake. Huu ni muundo ambao inakuwa ni rahisi sana
kwa Muungano kuvunjika.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Katika Rasimu ya Katiba, Serikali ya Muungano inapewa fursa ya kukopa kama chanzo cha kujipatia mapato ya kuendesha shughuli zake. Lakini, kwa sababu ya kukosa rasilimali zake yenyewe, huenda ikawa vigumu kwa Serikali hiyo kukopesheka. Kwa jumla hii ni Serikali ambayo ukuu wake hauna nguvu iliyo thabiti, na watu wengine wanaona kama vile ukuu huo haupo kabisa. Akitokea kiongozi ye yote wa nchi washirika akatunisha misuli dhidi ya Rais wa Muungano au kupinga maamuzi ya Serikali au chombo cha Muungano, Rais na Serikali yake watakuwa hawana lo lote la kufanya. Kwa kweli uhai wa Muungano katika muundo wa Serikali tatu ni wa mashaka makubwa.
Hofu hizi kuhusu udhaifu wa Serikali ya Muungano chini ya mfumo wa Serikali tatu unaopendekezwa, zinawasumbua hata wale wanaopendelea mfumo wa Serikali tatu kuwepo. Wao wangependa iwepo Serikali ya Muungano yenye nguvu na inayoweza kusimama yenyewe kwa kujitegemea. Wanaona kilichopendekezwa hakitoi matumaini hayo. Hii ina maana kuwa lazima mawazo bora zaidi yatolewe ili kupata Serikali ya tatu yenye ukuu unaoonekana na inayoweza kusimama yenyewe bila kuwa tegemezi na egemezi kwa nchi washirika. Pia inaweza kuwa nguzo ya kutegemewa na nchi washirika. Bila ya shaka Bunge hili likiamua tufuate mfumo huo linaweza kuonyesha njia ya kuondoa hofu hizo. Kwa waumini wa Serikali mbili wanaona kuwa huu ni uthibitisho wa ubora wa muundo wa Serikali mbili.

Changamoto za Hisia za Utaifa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Katika kuainisha changamoto za muundo wa Serikali tatu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeyataja mambo mengine mawili makubwa ambayo ningependa Waheshimiwa Wajumbe muyape tafakuri stahiki. Mambo hayo ni mosi, misuguano na mikwamo (deadlocks and paralysis) katika kujadili na kufanya uamuzi kuhusu mambo muhimu ya Muungano. Na pili, ni kuibuka kwa hisia za utaifa (nationalistic sentiments) wa zamani kwa nchi washirika. Nawaomba myatafakari kwa makini sana mambo haya, kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuhatarisha siyo tu ustawi na uhai wa Muungano, bali hata usalama wa raia na mali zao. Naona hata Tume haikuweza kupata ufumbuzi ulio mwafaka kabisa kwa changamoto hizi. Bila ya shaka katika mijadala yenu Waheshimiwa Wajumbe mnaweza kusaidia.

Ni lazima lifanyike kila linalowezekana kuhakikisha kuwa maamuzi hayakwami kwani yakikwama maana yake shughuli za Muungano zitakuwa zimekwama. Kama hazitakwamuliwa kwa wakati ustawi wa Muungano utaathirika. Ikishindikana kabisa kupatikana ufumbuzi Muungano unaweza kuvunjika. Kuibuka na kukua kwa hisia za utaifa (nationalistic feelings) kwa nchi washirika, yaani Utanganyika na Uzanzibari ni tishio kubwa sana kwa uhai wa Muungano. Hebu fikiria, watu walioishi pamoja kidugu na kwa kushirikiana, kama watu wamoja na raia wa nchi moja yaani Watanzania kwa miaka 50, kuja kujikuta uhusiano wao kuwa ni kati ya Watanganyika na Wazanzibari na siyo kati ya Watanznaia. Kwa mujibu wa sensa iliyopita takriban asilimia 90 ya Watanzania waliopo sasa wamezaliwa baada ya mwaka 1964. Nchi wanayoijua ni Tanzania.

Litakuwa ni jambo lenye mshtuko mkubwa na athari zisizoweza kutabirika,
watu hao watakapojikuta ni wageni wanaotakiwa kutengenezewa utaratibu maalum wa
kusafiri na kuishi wakiwa upande wa Muungano ambao siyo kwao kwa asili.
Wanakuwa wageni na fursa walizokuwa wanazipata waendapo popote haiwi rahisi
tena kuzipata.
Katika mazingira hayo ni rahisi sana chuki kupandikizwa na watu
waliokuwa ndugu mara moja watajikuta maadui. Aidha, watu wanaweza kujikuta
wakilazimika kurudi kwao kwa asili ama kwa kufukuzwa au kwa sababu ya mazingira
kuwa magumu kiasi cha kuona bora waondoke. Watu hao wanaweza kulazimika
kuondoka huku wakiacha nyuma kila kitu walichokichuma maishani.
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Changamoto hizi kubwa mbili za mfumo wa Serikali tatu ambazo Tume imeziona, ni za kweli. Si mambo ya kufikirika. Yale yaliyowakuta watu wenye asili ya Tanzania Bara ya kuchomewa moto biashara zao Zanzibar mwaka 2012 na watu wenye hisia kali za Uzanzibari, na kuwataka watu wa Bara waondoke Zanzibar, huenda yakawa madogo. Matukio ya namna hii yanaweza kutokea pande zote mbili na kusababisha maafa makubwa. Itaanza baina ya watu, baadaye itakuwa baina ya Serikali zetu mbili na kuzifikisha nchi zetu mbili zilizokuwa ndugu na rafiki, kwa nusu karne, ghafla kuwa maadui wasioombana chumvi na wasiotakiana heri. Umoja wetu utatetereka na Muungano wetu unaweza kuvunjika. Kwa nini tufike huko?

Sisi viongozi tuliopewa dhamana ya kuamua kwa niaba ya wananchi wetu, hatuna budi kuyapima mambo haya kwa umakini mkubwa ili tufanye uamuzi ulio sahihi. Tusije tukajutia uamuzi wetu tutakapoona watu wanafukuzana, wanauana na mali zao kuporwa. Na, tukifikia hatua hiyo Muungano kusambaratika halitakuwa jambo la ajabu.

Kwa kweli, unapoyatafakari haya, ni rahisi kuelewa
kwa nini wazee wetu waasisi waliamua walivyoamua. Waliona mbali. Tusipuuze
fikra zao na maono yao. Kuna hatari ya nchi yetu na watu wake kupoteza kila
kitu tulichokijenga kwa miaka 50. Badala ya kujenga tunaweza kujikuta tumebomoa
hata msingi katika nchi washirika. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka
1993 alituasa kuhusu hatari hiyo: “Hamuwezi kutenda dhambi kubwa namna hiyo
bila adhabu… na adhabu nyingine zimo mle mle ndani ya kitendo hazisubiri.”
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Siku moja kiongozi mmoja wa juu wa madhehebu ya dini nchini aliniuliza: “Hivi Serikali mbili zikiwa na matatizo jawabu ni kuongeza ya tatu? Si matatizo ndiyo yatazidi? Je, matatizo yakizielemea hizo Serikali tatu si kila mtu atachukua njia yake? Mtakuwa mmepoteza kila kitu. Mimi nawashauri msichoke kutafuta majawabu kwa matatizo ya hizi mbili! Huko mnakotaka kwenda kuna hatari nyingi”.

Pengine na ushauri huu wa mtu wa Mungu nao ni vyema kuupa nafasi na
kuutafakari.
Kazi Yenu Kubwa
Kazi Yenu Kubwa
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Mambo ya kuyasemea ni mengi mno lakini kwa sababu ya ufinyu wa muda, nisingeweza kuyazungumzia yote. Naamini, mtayaona katika kuipitia Rasimu na kwenye majadiliano yenu. Napenda kusisitiza kwenu kuwa kazi iliyo mbele yenu ni kubwa sana. Ni kubwa kwa maana mbili. Kwanza, jukumu lenyewe la kutunga Katiba ya nchi ni zito sana. Taswira ya nchi yetu itakuwaje na itaendeshwa vipi kwa miaka mingi ijayo iko mikononi mwenu. Ipeni nchi yetu hatima njema. Pili, ni kubwa kwa maana ya uzito wa mambo ya kujadili na kuyafanyia uamuzi. Kwa ajili hiyo, ni muhimu sana kuisoma Rasimu na Taarifa ya Tume kwa makini na kuzielewa. Jipeni muda wa kutafakari kila neno, kila sentensi, na kila dhana ili muweze kufanya uamuzi ulio sahihi. Mkifanya hayo mtakuwa mmeisaidia nchi yetu na Watanzania wote kupata Katiba nzuri.

Nimefarijika sana kusikia kuwa mtajigawa kwenye Kamati 12 wakati wa
kujadili Rasimu. Huu ni utaratibu mzuri kwani mkiwa katika vikundi vya watu
wachache, mtakuwa na mijadala ya kina zaidi. Watu wote wanaweza kupata fursa ya
kutoa maoni yao, kwa kila kifungu na kila jambo linaloibuliwa na kuzungumzwa.
Kwa kufanya hivyo, mtatimiza kwa ukamilifu jukumu lenu la kutunga Katiba. Wote
mtakuwa mmeshiriki kujadili kila sura na vipengele vyake vyote. Mkimaliza kazi
yenu mtapokea kwa haki sifa nzuri kama Katiba itakuwa nzuri, au lawama stahiki
iwapo itakuwa kinyume chake.
Pongezi kwa Mwenyekiti wa Muda
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama nitamaliza hotuba yangu bila ya kutambua kazi nzuri iliyofanywa na Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi, alipokuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hili. Kazi yake haikuwa rahisi hata kidogo, lakini kwa umahiri na ustadi mkubwa ameweza kufanikisha mambo kwa kiasi ambacho anastahili pongezi zetu sote. Anastahili pongezi kwa sababu yeye aliendesha Bunge hili bila ya kuwepo kwa kanuni. Tatizo hili hatakuwa nalo Mwenyekiti wa Kudumu kaka yangu Mheshimiwa Samuel Sitta.

Napenda pia kuwapongeza Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
kwa hatua mliyofikia. Hata hivyo, mmechukua muda mwingi katika hatua ya awali
hivyo hamna budi kuongeza kasi. Naomba niwakumbushe kuwa mijadala yenu hii
inafuatiliwa kwa karibu sana na Watanzania. Wamewekeza sana matarajio yao
kwenu. Hamna budi, haiba na taswira ya uongozi muionyeshe wakati wote wa
kuendesha mijadala yenu kwa lugha na vitendo vyenu. Wakati wa semina na mjadala
wa kupitisha Kanuni za Bunge hili, baadhi ya wananchi wamekwazika sana na
mwenendo wa baadhi ya Wajumbe. Hawakutegemea kuyaona matendo waliyoyaona
mkifanya na kusikia maneno waliyoyasikia kutoka kwenye vinywa vya baadhi yenu.
Ni matumaini yangu na ya Watanzania wote kuwa hali ile haitajirudia tena
katika awamu hii. Tusiwafikishe mahali Watanzania wakakata tamaa na Wajumbe wao
au na hata chombo hiki muhimu sana kwa mustakabali wao na wa nchi yao. Tutoe
hoja badala ya kupiga kelele (argue don’t shout) au kuzomea. Hakuna haja ya
kutumia lugha isiyokuwa ya staha katika kujieleza. Hakuna haja ya kukingiana
ngumi, kutishiana hili na lile au hata kugombana. Ni utovu wa uungwana
usiotegemewa kutoka kwenu. Tusiwaangushe wananchi wa Tanzania wanaotutegemea
sana.
Wekeni Maslahi ya Taifa Mbele
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Ombi langu la mwisho kwenu ni kuwasihi kuwa wakati wote muongozwe na kujali maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake badala ya kujali maslahi yenu binafsi au ya makundi yenu. Naomba kaulimbiu yenu iwe “Tanzania Kwanza”. Najua kila mmoja wenu amekuja na maoni yake au atakuwa nayo kwa kila jambo litakalojadiliwa. Wengine wamepewa misimamo na vyama vyao au makundi yao. Si jambo baya na ni hatua muhimu ya kuleta mafanikio, kama misimamo hiyo na mawazo hayo ni ya kujenga.

Hata hivyo, mnachotegemewa kufanya ni kuwa tayari
kuwianisha na kuunganisha mawazo yenu mazuri na ya wenzenu, ili kupata msimamo
wa pamoja na uamuzi wa pamoja ulio bora. Kwa sababu hiyo, hamna budi kuwa
tayari kusikiliza mawazo ya wengine, hata kama ni tofauti na yenu mliyokuja
nayo. Tafuteni kilicho chema kwa yale yanayosemwa na watu wengine hata kama ni
watu usiokubaliana nao au huwapendi au hampendani. Kunaweza kuwepo kitu chenye
manufaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe;
Nawaomba muwe hodari wa kushawishi badala ya kulazimisha. Mkifanya hivyo hamtalazimika kutumia muda mwingi wa kula njama za namna ya kuwazidi maarifa wale mnaotofautiana nao kwa mawazo. Lazima pia mtafute namna ya kushirikiana na kuwasiliana na makundi mengine. Msitafute kushindana, hili ni jambo ambalo lazima wote mtoke hapa mkiwa washindi. Yaani lazima Watanzania wote washinde kwani wao ndiyo wenye Katiba yao. Nawapongeza viongozi wa vyama vya siasa na asasi mbalimbali kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa kuwa na taratibu za mawasiliano, mashauriano na ushirikiano. Daima muwe watu wa kutafuta maridhiano. Mmefanya vizuri katika hatua ya awali. Mmejiwekea taratibu nzuri za kufanya hayo, tafadhalini zitumieni. Jengeni madaraja imara zaidi katika awamu hii.

Naomba nimalize kwa kuwaomba Watanzania wote tukiongozwa na viongozi wetu wa dini tumuombe Mola wetu ajalie rehema zake ili mchakato wa kutunga Katiba uende salama. Aliongoze Bunge hili na Wajumbe wake waweze kufanya uamuzi ulio sahihi na wenye manufaa kwa taifa letu kwa kila watakaloliamua.

Baada ya kusema maneno yangu mengi hayo, nirudie kukushukuru Mheshimiwa
Mwenyekiti kwa kunipa fursa hii adhimu ya kulihutubia Bunge Maalum la Katiba.
Nawatakieni kila la heri na mafanikio mema. Katiba Mpya Inawezekana, Timiza
Wajibu Wako.
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Libariki Bunge Maalumu la Katiba!
Mungu Libariki Bunge Maalumu la Katiba!
Asanteni sana kwa kunisikiliza!
Subscribe to:
Posts (Atom)