Thursday, June 21, 2007

Serikali ya Ufaransa yaogopa Black Berry


Serikali ya Rais Nicolas Sarkozy imepiga marufuku mawaziri na wengine wote wanaohudhuria vikao vya serikali kutumia simu za mkononi aina ya BlackBerry. Sababu za kupigwa marufuku matumizi ya simu hizo ni kuogopa kusikilizwa simu hizo na Wamarekani. Serikali hiyo ikifuatilia ushauri wa mamlaka ya usalama wa taifa ya Ufaransa, SGDN, kuwa simu hizo mitambo ya huduma ya simu hizo iko Marekani na Uingereza na kuwa simu hizo zina matatizo ya kiusalama. Viongozi hao Ufaransa wanatakiwa kuingia kwenye mikutano na kuziweka simu zao mezani na kutoa betri!!! Si Wafaransa tu, hata Waholanzi nao wana wasiwasi na usalama wa simu hizo. Tahadhari hizo zimetolewa na idara ya usalama wa taifa ya Uholanzi, AIVD. Siyo tu Wafaransa na Waholanzi tu ndio waoga, hata mabenki makubwa nchini Marekani kwenyewe yanaogopa kutumia Black Berry wanapokuwa na vikao vyao...
Chanzo cha habari:
Imetumwa na Omari Guy Agallo Chichi.


No comments: