Tuesday, June 12, 2007
Watano washtakiwa kwa kula rushwa hapa Oslo!
Watu watano wamefunguliwa mashtaka mjini Oslo na Kitengo Maalumu cha Polisi cha Kupambana na Uhalifu wa Kuhujumu Uchumi na Mazingira "The Norwegian National Authority for Investigation and Prosecution of Economic and Environmental Crime" au "Økokrim" kwa Kinorwejiani. Mmoja wa hao waliokamatwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni moja kubwa hapa Oslo. Amefunguliwa mashtaka ya kuiba Kroner milioni 12 za kampuni na Kroner milioni mbili, laki saba za ongezeko la bei ya thamani na kujaribu kubatilisha ankra za matumizi na mapato ya kampuni.
Mwendesha mashtaka wa Økokrim, Bw. Petter Nordeng akihojiwa na http://www.na24.no/ alisema jamaa huyo ametumia wafanyakazi hewa na bubu kwenye kandarasi alizochukua na baadaye kuwasilisha risiti batili kwa malipo.
Hao wengine wanne wanashtakiwa kwa kujaribu kutumia hela zilizopatikana kwa njia zisizo halali kwa ajili ya biashara halali na wizi wa hela za ongezeko la bei ya thamani (Value Added Tax) kiasi cha Kroner milioni 10.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment