
Mzee wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Mvuti Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, Phares Kweka wiki hii alikumbwa na aibu ya mwaka baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa rafiki yake aitwaye Nasim Mohamed katika nyumba ya kulala wageni (gesti) ya Mremi’s iliyopo Buguruni jijini.
Tukio hilo lilitokea saa nne, Jumatatu ya Septemba 17, mwaka huu baada ya kuwekewa mtego na mume wa mwanamke huyo aitwaye Marc Tibber uliofanikisha kumnasa akiwa mtupu kitandani kama anavyoonekana pichani ukurasa wa mbele......
Habari za awali kutoka kwa chanzo chetu, (jina tunalihifadhi) zilidai kuwa mzee huyo wa kanisa ambaye ni rafiki mkubwa wa Tibber alianza kumtongoza mwanamke huyo tangu mwaka 2004 ambapo hakuweza kufanikiwa kutokana na kukataliwa.
Habari zaidi zinasema pamoja na kukataliwa Kweka hakukata tamaa kwani alimuahidi kupatia shilingi laki tatu (300,000) ili aweze kumkubalia kufanya naye mapenzi.
“Mzee huyo wa kanisa alimwambia kuwa pesa hizo angeweza kumpatia ndani ya gesti endapo angemkubalia kufanya naye mapenzi,” kilisema chanzo hicho.
Mtoa habari huyo ambaye ni mtu wa karibu wa Tibber alisema kuwa Nasim, hakufurahishwa na kitendo cha kiongozi huyo wa kanisa kumtaka kimapenzi, hivyo mwanamke huyo alimtaarifu mumewe na ndipo mpango wa kumnasa ulipoanza.
“Baada ya mumewe kupata taarifa hiyo walikaa na mkewe na kupanga mikakati ya kumshikisha adabu hasa ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja kati ya viongozi wa kanisa wanaotakiwa kulinda maadili mema ya kanisa na katika jamii,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, habari zinasema kuwa mikakati hiyo ni pamoja na kuwatonya waandishi wa habari ambao walitakiwa kufika katika gesti hiyo na kushuhudia fumanizi hilo.
Awali mzee huyo wa kanisa walikubaliana na mwanamke huyo kukutana katika gesti hiyo siku ya Jumatatu ya Septemba 17 saa 4.00 asubuhi wakati mumewe akiwa kazini na kumuahidi kumpa shilingi laki mbili ‘keshi’ mara baada ya kumaliza shughuli na laki moja iliyobaki angeitoa siku nyingine.
“Walichukuwa chumba namba 21 na kuwasiliana na mumewe kila hatua iliyokuwa ikiendelea chumbani huku mumewe akiwapitia waandishi wa habari na kusogea nao sehemu ya tukio,” kilisema chanzo hicho.
Habari zinasema akiwa chumbani, Kweka aliagiza bia mbili na kuanza kukata kiu huku akiwa ameshavua nguo zake, ambapo Tibber pamoja na waandishi hao walitinga ndani baada kupewa ishira kwa njia ya simu.
Waandishi wetu na mwenye mke walipotinga chumbani humo, walimkuta mzee mzima akiwa mtupu kitandani huku mwanamke akijifanya anavua nguo na kufanikiwa kupiga picha kadhaa zikiwemo za video kama ushahidi.
Hata hivyo, Kweka alipoulizwa kwanini anamsaliti rafiki yake wakati yeye ni mtumishi wa Mungu, hakuwa na la kusema zaidi ya kuwakodolea macho waandishi wetu kama mtu aliyenaswa na umeme.
Akiongea na baadhi ya watu waliokuwepo kwenye tukio hilo, Tibber alisema kuwa amemsamehe Kweka kwani yaliyopita yamepita. “Yaliyopita yamepita, tugange yajayo,” alisema.
Aidha waandishi wetu walikwenda Mvuti kwenye kanisa hilo na kumtafuta kiongozi ili aeleze kama anamfahamu Kweka lakini hawakumkuta.
Hata hivyo, baadhi ya waumini walisema kuwa wanamfahamu mzee huyo kuwa ni mmoja wa viongozi (wazee) wa kanisa wanaotegemewa katika kulinda maadili kanisani hapo.
Kutoka: Global Publishers Tanzania.
No comments:
Post a Comment