Friday, October 05, 2007

Danny Glover kaiba mwandiko wa Med Hondo!

Med Hondo

Danny Glover

Nimesoma habari ya kusikitisha sana. Mcheza sinema Danny Glover, eti kaiba script (mwandiko) ya Mtunzi Med Hondo (Mohammed Abid Hondo). Hiyo script inahusu mapinduzi kule Haiti. Weusi wa Haiti walitwaa uhuru wao kutoka kwa wazungu zaidi ya miaka 200 iliyopita. Kiongozi wao alikuwa Toussaint Louveture. Hapa USA wacheza sinema wengi wamezungumiza na kutuma resumes na headhsots zao, nikiwemo mimi ila kupata nafasi ya kucheza katika sinema hiyo ya kihistoria.

Danny Glover na kampuni yake walikuwa wanafanya maandalizi ili ipigwe hivi karibuni. Sasa inaelekea itakuwa kesi mahakamani. Labda Glover akubali kuwa Med Hondo ndo alikuwa na Original Idea na kumpa heshima yake.

Moja ya sinema ya Med Hondo ni Sarraounia ambayo ilikuwa moja wa sinema maarufu za kiafrika miaka ya 80.

Sinema ya Toussaint itachezwa na akina Don Cheadle, Angela Bassett, Wesley Snipes, Mos Def , Chiwetel Ojiofor na wengine.

Chini ni barua ya wazi kutoka kwa Med Hondo, kwa Danny Glover. Kuona na cheti cha usajili bofya hapa: http://www.medhondo.com/menuactualite.html

Toka kwa dada Chemi Che Mponda: http://swahilitime.blogspot.com/



No comments: