Friday, October 12, 2007


Haya walipa kodi wa Norway....

Orodha ya walipa kodi wote wa Norway imeshawekwa mtandaoni. Unaweza "kumchungulia" jirani yako, ama ndugu na jamaa ujue mwaka 2006 alichuma kroner ngapi na alilipa kodi kiasi gani!!!!! Hapa Norway orodha kama hizi zinamwagwa waziwazi watu wajionee.

Watu wengi wamekuwa wakipinga kuwekwa kwenye kadamnasi orodha ya walipa kodi. Walalahoi na walalahai wanasema kuwa nani anachuma kroner ngapi na analipa kodi kiasi gani kwa mwaka ni masuala ya binafsi hivyo hayapaswi kujulikana na umma wote wa ndani na nje ya nchi.
(kwa Kinorwejiani tu)
.

Baadhi ya mitandao imeshazifuta viungo walivyoviweka vya kuangalia mapato na kodi za watu hapa Norway. Norway ni nchi pekee duniani "inayoanika" orodha ya walipa kodi. Gongola kwenye hivyo viungo hapo chini.

http://tjenester.skatteetaten.no/


http://skatt.vg.no/

http://www.dagbladet.no/skatt/

Viungo vyote viwili kwa Kinorwejiani.


No comments: