Wednesday, October 10, 2007

KIPANYA NA FINA MANGO


Ukiwa jijini Dar-es-salaam na kwingineko popote inaposikika Clouds FM (88.4) nchini Tanzania na ukafungulia redio yako kuanzia saa 12 mpaka saa 3 asubuhi, watangazaji Ali Masoud maarufu kama Masoud Kipanya (pichani aliyesimama) na Fina Mango (aliyeketi) watakusaidia kuianza siku yako vyema kwa habari mbalimbali zinazoambatana na burudani. Kipindi chao kinaitwa Power Breakfast.

Masoud Kipanya pia ni mbunifu wa mitindo (fashion designer) na mchora katuni matata sana. Katuni yake ya Kipanya inapatikana ndani ya gazeti la Mwananchi na pia kwenye tovuti yake. Masoud alikuwa ni mmojawapo wa watu maarufu nchini Tanzania (bongo celebrities) tuliofanya nao mahojiano mwanzo mwanzo blog hii ilipoanzishwa. Mahojiano hayo bado yanapatikana hapa mtandaoni. Unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.





No comments: