Tuesday, January 29, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Kundi B


Mali mdebwedo kwa

Ivory Coast, yafungwa 3 - 0

Ivory Coast (Les Éléphants/The Elephants) wameingia robo fainali wakiwa na pointi 9 baada ya kuwafunga Mali (Les Aigles/The Eagles) kwa magoli 3 - 0. Didier Drogba alifungua mlango baada ya kufunga goli la kwanza kwenye dakika ya 10. Alipokea pasi safiii toka kwa Yaya Toure. Goli la pili la Ivory Coast lilifungwa na Marc Zoro. Goli la tatu lilifungwa na Sanogo. Ivory Coast inacheza na Guinea, siku ya Jumapili, tarehe 3.2.2008.


Shabiki wa Ivory Coast


Mashabiki wa Benin


Mchezaji wa Ivory Coast akimbabaisha mchezaji wa Mali.


Frederic Kanoute (kulia wa Mali) akizidiwa na mchezaji wa Ivory Coast.

Timu zilikuwa kama ifuatavyo:

Ivory Coast: Barry, Eboue, Zokora, Fae, Zoro, Romaric, Tiene, Toure Yaya, Keita (Bakari Kone 59), Arouna Kone, Drogba (Sanogo 75). Marezevu: Tiassa Kone, Loboue, Gohouri, Boka, Meite, Toure, Dindane, Gervinho, Kalou, Djakpa.

Magoli ya Ivory Coast yalifungwa na: Drogba 10, Zoro 54, Sanogo 86

Mali: Mahamadou Sidibe, Adama Coulibaly (Diallo 47), Kante, Tamboura, Sammy Traore, Drissa Diakite, Keita, Djibril Sidibe, Toure (Dissa 60), Kanoute (Mohamed Sissoko 46), Dramane Traore. Marezevu: Soumalia Diakite, Oumar Sissoko, Moussa Coulibaly, Dembele, Amadou Sidibe, Kone, Diamoutene, Mamady Sidibe.

Aliyepewa kadi ya njano: Tamboura.

Refarii: Eddy Maillet (Seychelles).



Nigeria yaingia robo fainali,

yaifunga Benin 2 - 0

Nigeria (The Super Eagles) imefanikiwa kuingia robo fainali kibahati sana, baada ya kuifunga Benin (Les Écureuils/The Squirrels) magoli mawili kwa sifuri. Nigeria wanaingia robo fainali kwa kuwa na pointi 4 na wamewatoa Mali nao pia wakiwa na pointi 4. Tofauti ya magoli ndiyo inayowafanya Nigeria kuendelea. Nigeria itacheza wapinzani wao wa jadi, Ghana kwenye robo fainali.


Shabiki wa Nigeria (The Super Eagles)


Ike Uche wa Nigeria akimtoka mchezaji wa Benin.

The Super Eagles wakishangilia kuingia robo fainali.

Timu zilikuwa kama ifuatavyo:

Nigeria: Ejide, Yobo, Nwaneri, Shittu, Taiwo, Etuhu (Eromoigbe 74), Uche, Obi, Utaka (Obinna 52), Odemwingie (Afolabi 90), Yakubu. Marezevu: Enyeama, Kanu, Martins, Olofinjana, Makinwa, Emeghara, Okonkwo, Apam, Aiyenugbu.

Aliyepewa kadi ya njano: Odemwingie.

Magoli ya Nigeria yalifungwa na: Obi 53, Yakubu 86.

Benin: Amoussou, Gaspoz, Adenon, Chrysostome, Adjamossi (Ogunbiyi 46), Boco, Ahoueya, Oketola, Sessegnon (Maiga 84), Omotoyossi, Oumar Tchomogo. Marezevu: Chitou, Koukou, Traore, Rouga, Seka, Djidonou, Seidath Tchomogo, Oladipikpo, Soglo, Ouzerou.

Aliyepewa kadi ya njano: Oketola.


No comments: