Thursday, January 31, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Kundi C


Kameruni 3

Sudan 0

Eto´o aweka historia


Kameruni (The Indomitable Lions) imeingia kwenye robo fainali baada ya kuifunga Sudan (Sokoor Al-Jediane/Desert Hawks) kwa magoli 3 - 0. Kwenye mechi hii, mchezaji Samuel Eto´o ameweka historia kwenye fainali za mataifa ya Afrika, kufunga goli la 15 kwenye mechi zote alizocheza kwenye fainali za mataifa ya Afrika. Alifunga goli hilo la kihistoria kwa penalti kwenye dakika ya 27. Rekodi ya zamani ilikuwa inashikiliwa na Laurent Pokou wa Ivory Coast (miaka ya 1970) ya magoli 14. Timu zilikuwa hivi:

Kameruni: Kameni, Song, Atouba (Tchato 46), M'Bami, Geremi, Eto'o, Emana (Tomou 57), Epalle (Essola 76), Song Billong, Job, Bikey. Marizevu: Angbwa, Binya, Hamidou, Idrissou, Makoun, Mbarga, Mbia, N'Guemo, Nkong.

Aliyepewa kadi ya njano: Bikey.

Magoli ya Kameruni: Eto'o 28 pen, Ali Elkhidir 34 (Msufani alijifunga), Eto'o 90.

Sudan: Elmuiz Abdalla, Bakhit (Tahir Osman 54), El Tayeb, Ali Elkhidir, Yousif Hado, Kuku, Lado, Karar, El Bashir, Kamal Tambal (Hassan 77), Agab Sido (Babiker 62).
Marizevu: Bader Eldin Abdalla, Ahmed, Ali Idris Farah, El Basha Adam, El Hadi Salem, Eldin Ahmed Gibril, Hameed Amari,

Aliyepewa kadi ya njano: Yousif Hado.


Samuel Eto´o baada ya kufunga goli la kihistoria.


Yousef Alaeldin (Sudan, jezi nyeupe) akimtoka mchezaji wa Kameruni


Kipindi cha pili, Sudan walijitahidi kuwazuia Wakameruni.



Misri 1

Zambia 1


Kwenye mechi nyingine kwenye kundi hili, Misri (The Pharaohs) walitoka sare na Zambia (Chipolopolo). Kameruni na Misri zinaingia robo fainali kwenye kundi hili. Timu zilikuwa hivi:

Misri: El Hadari, Mohamed, Hany Said, Moawad, Gomaa, Fathi, Abd Rabou, Shawky, Hassan (Aboutrika 60), Moteab (Ibrahim Said 77), Zaki (Zidan 60).
Marizevu: Abdel Monssef, Sobhy, El Saeed, Fathallah, El Mohamady, Gamal, Mostafa, Shaaban, Fadl.

Alyefunga goli: Zaki dakika ya 15.

Zambia: Mweene, Musonda, Himonde, Mwanza (Kampamba 30), Hachilensa, Chansa (Kalaba 77), Bakala, Felix Katongo, Christopher Katongo, Jacob Mulenga (Phiri 65), Chamanga.
Marizevu: Poto, Kakonje, Chinyama, Nketani, Kasonde, Clifford Mulenga, Njovu, Mayuka, Sunzu.

Waliopewa kadi za njano: Felix Katongo, Chansa.

Aliyefunga goli: Christopher Katongo 88.

Refarii: Koman Coulibaly (Mali).


Amr Zaki (Misri) akifunga goli dakika ya 17 ya mchezo.


Felix Katongo (Zambia) aliwapa shida sana mabeki wa Misri kama inavyoonyesha hapa.


Chris Katongo (nduguye Felix Katongo) naye alikuwa tishio kwa mabeki wa Misri.


Mechi zilichezwa Jumatano, 30 Januari 2008



No comments: