Gavana Ndulu afanya
Mabadiliko Benki Kuu..
Mabadiliko Benki Kuu..
Gavana Profesa Benno Ndulu pichani,amefanya mabadiliko makubwa ndani ya taasisi hiyo nyeti ya fedha nchini kwa kupangua safu ya wakurugenzi wa Idara mbalimbali.
Mabadiliko hayo ambayo ni ya kwanza kufanywa na GAvana Ndulu tangu ateuliwe kushika wadhifa huo wiki iliyopita, yamemng'oa mmoja wa vigogo wa benki hiyo Amatus Liyumba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA).
Profesa Ndulu alimtaja Leornad Kasalika kutoka BoT tawi la Arusha kuchukua nafasi ya Liyumba.
Gavana Mpya Nduru ambaye amekuwa akiangaliwa kama mwenye kuweza kuleta mabadiliko ndani ya BoT kutokana na uzoefu wake wa kufanya kazi Benki ya Dunia (WB) alisema kwamba mabadiliko hayo yamegusa idara za makao makuu na matawi yote ya benki hiyo, isipokuwa Mwanza.
Profesa Ndulu aliongeza kwamba katika mabadiliko hayo, baadhi ya wakurugenzi wamepandishwa, wengine kuondolewa na baadhi kuhamishwa idara.
Hata hivyo, Profesa Ndulu alisema taarifa zaidi kuhusu idara na majina ya watu walioteuliwa zitatangazwa wakati wowote kuanzia sasa.
Ingawa hakutaja majina zaidi, alisema wakurugenzi watano ni wapya ambao wamepandishwa. Alisema mabadiliko hayo pia yameondoa watu ambao walikaa muda mrefu katika idara zao, kupandisha vijana na kuleta uwiano wa rika la uongozi kwa kuzingatia sifa zinazostahili.Habari hiii na Ramadhan Semtawa.
Chanzo cha habari: http://haki-hakingowi.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment