Sunday, June 22, 2008


Andrei Arshavin akiwanyamazisha wapenzi wa Uholanzi baada ya kufunga goli


Dimitri Torbinski akifunga goli


Edwin van der Sar (kipa wa Uholanzi) akiwa na majonzi baada ya kutolewa kwenye robo fainali


Kocha wa Urusi, Guus Hiddink (Mholanzi) akishangilia ushindi na kipa Igor Akinfeev na Sergei Ignashevich.


Urusi yaitoa Uholanzi

Urusi 3 – Uholanzi 1

Baada ya dakika 120


Urusi imeitoa Uholanzi kwenye robo fainali, baada ya dakika 12o kwa kuwafunga 3 – 1. Uholanzi timu iliyopewa nafasi kubwa ya kushinda kombe la mataifa ya Ulaya, ilijikuta ikipachikwa goli la kwanza kwenye dakika ya 55 na Pavlyuchenko. Uholanzi ilisawazisha kwenye dakika ya 86 na Van Nistelrooy. Ikabidi ziongezwe dakika 30 za ziada. Urusi ilipata goli la pili dakika ya 112 lililofungwa na Torbinsky na kwenye dakika ya 116 Warusi walivunja matumaini ya Waholanzi kwa kuandika goli la tatu na Arshavin. Kocha wa Uholanzi, Van Basten ametangaza hata kabla ya fainali hizi kuwa anajiunga na AFC Ajax, naye kipa wa Uholanzi Van der Sar amesema kuwa mechi hii ni yake ya mwisho ya kimataifa.



No comments: