Monday, June 23, 2008




Kipa Iker Casillas (Hispania) na Gianluigi Buffon (Italia) kabla ya mechi

Marcos Senna (kulia) akikabiliwa na Massimo Ambrosini


Iker Casillas (kipa) Hispania akiokoa penalti


Hispania 4 – Italia 2

Baada ya dakika 120

na penalti

Tarehe 22 Juni ni tarehe ya balaa kwa soka la Hispania kwenye mashindano ya kimataifa. Mara tatu Hispania imetolewa kwenye mashindano makubwa kwa penalti kwenye tarehe 22 Juni. Mara ya kwanza walipocheza na Ubelgiji kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 1986. Mwaka 1996 walitolewa tena kwa penalti na Uingereza tarehe hii hii. Na mara ya mwisho ilikuwa 2002 fainali za kombe la dunia nchini Korea Kusini/Japan walipotolewa na Korea Kusini. Mara ya mwisho kwa Hispania kuifunga Italia ilikuwa mwaka 1920. Baada ya dakika 120 kumalizika Hispania na Italia zilikuwa suluhu 0 – 0.

Penalti

Hispania ilifunga magoli 4 yaliyofungwa na Villa, Cazorla, Senna na Fabregas. Italia ilifunga magoli mawili kwa penalti za Grosso na Camoranes. Casillas kipa wa Hispania aliokoa penalti zilizopigwa na De Rossi na Di Natale. Buffon kipa wa Italia alipangua penalti moja ya Hispania iliyopigwa na Guiza.




No comments: