Thursday, June 12, 2008


Kundi B

Ujerumani yashindwa

Kufurukuta mbele ya Kroatia

Kroatia 2 = Ujerumani 1

Ujerumani imekuwa na matatizo ya kuifunga Kroatia kwenye michezo ya kimataifa. Historia imejirudia tena baada ya Kroatia kuifunga Ujerumani kwa magoli 2 – 1 kwenye uwanja wa Hypo-Arena mjini Klagenfurt. Magoli ya Kroatia yalifungwa na Srna dakika ya 23 na Olić dakika ya 62. Goli la kufutia machozi la Ujerumani lilifungwa na Podolski dakika ya 79. Kabla mpira kwisha, Bastian Schweinsteiger alipewa kadi nyekundu dakika ya 90 baada ya kumsukuma kwa nguvu mchezaji wa Kroatia.


Slaven Bilic, kocha wa Kroatia akishangilia ushindi


Kocha wa Ujerumani Joachim Löw baada ya kufungwa na Kroatia


Kiungo wa Ujerumani Michael Ballack akionyesha ufundi wake wa kulisakata kabumbu.


Luka Modrić akishangilia ushindi dhidi ya Ujerumani

Kiungo wa Kroatia Ivan Rakitic akimtoka mlinzi wa Ujerumani

Austria wanusurika

dakika za majeruhi!

Poland 1 = Austria 1

Austria imeponea chupuchupu kutolewa kwenye fainalia kama ilivyotokea jana kwa wenyeji washiriki wenzao Uswisi jana. Austria walianza kwa mashambulizi makali kwenye goli la Poland, bahati haikuwa yao. Badala yake ilikuwa Poland iliyopata goli la kwanza kwenye dakika ya 30 na Roger Guerreiro (Mpolish mwenye asili ya Brazil). Austria hawakukata tamaa. Kwenye dakika ya 92 (dakika ya 2 ya majeruhi) walipata penalti baada ya mchezaji wa Austria kushikwa jezi na kuangushwa kwenye goli la Poland. Ivica Vastic hakufanya makosa, akafunga. Austria wana nafasi ya kuingia robo fainali kama watawafunga Ujerumani. Mechi hii ilichezwa Ernst Happel Stadion



Kiungo wa Poland Roger Guerreiro akijaribu kumtoka Gyorgy Garics (Austria)


Mshambuliaji wa Poland Roger Guerreiro akikumbatiwa na wenzake baada ya kufunga goli.



No comments: