Tuesday, June 10, 2008



Kundi C

Sweden 2 = Ugiriki 0

Mabingwa wa Ulaya (mwaka 2004) Ugiriki wameshindwa kuonyesha makali yaliyowafanya wawe mabingwa miaka minne iliyopita, baada ya kufungwa na Sweden (Blågult /yellow and blues) magoli 2 – 0. Goli la kwanza la Sweden lilifungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 67 baada ya kupewa pasi na Henrik Larsson. Goli la pili lilifungwa na Petter Hansson kwenye dakika ya 72.


Zlatan Ibrahimovic akishangilia goli alilofunga


Wachezaji wa Sweden wakimshangilia PetterHansson baada ya kufunga goli la pili


Mashabiki wa Sweden.


Hispania 4 = Urusi 1

Hispania ni timu inayopewa nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa wa mataifa ya Ulaya mwaka huu. Ikicheza na wachezaji vijana na maarufu kama Fernando Torres; Cesc Fabregas, Raul na David Villa wameifunga Urusi magoli 4 – 1. Magoli ya Hispania yalifungwa na David Villa (magoli 3) na Cesc Fabregas (goli 1). Goli la kufutia machozi la Urusi lilifungwa na Roman Pavlyuchenko.


David Villa akishangilia moja ya magoli aliyofunga


David Villa akikumbatiwa na Fernando Torres baada ya kufunga goli


Picha zote toka Getty Images




No comments: