Kundi C
Kweli Ijumaa tarehe 13
ni siku ya balaa
Uholanzi yaibamiza
Ufaranza 4 – 1
Kwa mara nyingine tena Uholanzi wameonyesha kuwa wanataka kukopi mafanikio yao ya mwaka 1988, kwa kuifunga Italia. Uholanzi ikicheza kwa kasi na kwa uhakika, ilianza kwa kupata goli la kwanza kwenye dakika ya 9 lilifoungwa na Dirk Kuyt kwa kichwa baada ya kona. Goli la pili la Uholanzi lilifungwa na Robin van Persie kwenye dakika ya 58. Dakika ya 71 Thierry Henry alifunga goli la kufutia machozi. Kabla Ufaransa hawajafuta machozi vizuri, Robben akawavunja nguvu kwa kufunga goli la tatu kwenye dakika ya 72. Dakika ya 90, Wesley Sneijder alipokea pasi safi akageuka kiufundi na kupiga shuti kali na kuwamaliza kabisa Wafaransa. Goli la nne! Uholanzi wanaingia robo fainali kama washindi wa kwanza kundi hili. Mechi ya mwisho kwenye kundi hili itachezwa Jumanne 17 Juni.Uholanzi itachuana na Romania na Ufaransa na Italia. Mechi hii ilichezwa uwanja wa Stade de Suisse mjini Berne.
Kiuongo wa Uholanzi Wesley Sneijder akifunga goli la nne
Robben akishangaliwa na Wesley Sneijder ba Robin van Persie baada ya kufunga goli la tatu
Thierry Henry baada ya kufunga goli la kufutia machozi
Robin van Persie akishangilia baada ya kufunga goli la pili
Dirk Kuyt akifunga goli la kwanza la Uholanzi
Italia yaokolewa na
Gianluigi Buffon.
Romania 1 = Italia 1
Mabingwa wa dunia Italia, imejiweka kwenye nafasi ngumu ya baada ya kutoka sare na Romania. Romania ndio waliokuwa wa kwanza kufunga kwenye dakika ya 54 lililofungwa na Adian Mutu. Haikuchukua muda, Italia ilisawazisha kwa goli la Panucci (Panuchi). Kwenye dakika ya 81, Romania walipata penalti, kipa Gianluigi Buffon alipangua penalti ya Mutu! Italia, Romania na Ufaransa zinatakiwa kushinda kwenye mechi zao za mwisho Jumanne wiki ijayo ili kuwa na uhakika wa kuingia robo fainali. Mechi hii ilichezwa Letzigrund mjini Zurich.
Gianluca Zambrotta akimpongeza Buffon kwa kuokoa penalti ya Adrian Mutu
Giorgio Chiellini (Kulia) akijaribu kumtoka Daniel Niculae (Romania, kushoto)
Fabio Grosso (Italia) akijaribu kuwatoka Cristian Chivu Nicolae Dică (Namba 5 na 20 Waromania)
Picha kutoka AFP na Getty Images.
No comments:
Post a Comment