Saturday, June 21, 2008


Semih Şentürk (Uturuki) akifunga goli

Semih Şentürk (Uturuki) jinsi alivyofunga goli sekunde 10 baada ya dakika 30 za nyongeza kwisha.

Semih Şentürk (Uturuki) akiwanyamazisha wapenzi wa Kroatia

Uturuki yafanya tena

maajabu!

Uturuki 4 – Kroatia 2

Baada ya dakika 120

na penalti


Kroatia ndiyo iliyokuwa imepewa nafasi kubwa ya kuifunga Uturuki. Hadi dakika 90 timu zilikuwa sare bila kufungana. Zikaongezwa dakika 30. Ikiwa imebakia dakika moja mpira kwisha, Kroatia walipata bao lililofungwa na Klasnic. Kroatia wakijua kuwa ushindi uko mfukoni mwao. Uturuki hawakukata tamaa. Pamoja na kipa wao, walishambulia goli la Kroatia kama nyuki. Golikipa wa Uturuki Rustu alipiga shuti la mbali na katika purukushani, Semih Şentürk, akaupokea mpira na kushuti goli la fainali hizi!!!! Uturuki 1 – Kroatia 1

Penalti.

Kroatia ndio waliokuwa wa kwanza kupiga penalti. Modric akapiga nje. Arda akafunga kwa uturuki. Srna (kroatia) akafunga. Semih (Uturuki) akafunga. Rikitic (Kroatia) akapiga nje. Altintop (Uturuki) akafunga. Pedric (Kroatia) akapiga na kipa wa Uturuki, Rustu akaokoa!

Uturuki inacheza na Ujerumani kwenye nusu fainali.





No comments: