Ujerumani 3 – Uturuki 2
Nusura Uturuki
Uturuki imetolewa kwenye fainali hizi, lakini imejiongezea wapenzi wa soka duniani kwa jinsi timu yao ilivyokuwa inacheza kwa moyo wa pamoja na wa kujituma sana. Kipindi cha kwanza kilitawaliwa na Uturuki na walipata goli la kwanza, baada ya Kassim Kassim kupiga tikitaka na kuogonga mwamba wa goli la Ujerumani na Ugor Boral akafunga dakika ya 22. Goli hili liliwaamsha Wajerumani. Wakafanya mashambulizi makali na dakika 26 wakasawazisha kwa goli la Schweinsteiger, baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Podolski.
Dakika ya 79 Miroslav Klose alifunga goli la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Philipp Lahm. Kama kawaida yao kwenye fainali hizi, Waturuki hawakukata tamaa. Wakaanza mashambulizi ya nguvu na yalizaa matunda kwenye dakika 86, beki wa Uturuki Sabri Sarioglu alipomtoka beki wa Ujerumani na kutoa pasi, Semih Senturk akaupinda mpira kiustadi na kumwacha kipa Lehmann akienda kuutoa mpira nyavuni!
"Ujerumani ni Ujerumani mtacheza weee mnavyoweza dakika 90 mshindi ataibuka Ujerumani" nikinukuhu maneno ya Gary Lineker mchezaji wa England miaka kadhaa iliyopita na ndiyo ilivyotokea kwenye nusu fainali hizi, Philipp Lahm alifunga goli murua baada ya kucheza pasi safi na Thomas Hitzlperger. Ujerumani imeibuka mshindi kwa kuitoa Uturuki na inaingia kwenye fainali. Shilingi yangu naiweka kwa Wajerumani kuwa wanaibuka washindi wa fainali hizi!!!
No comments:
Post a Comment