Friday, July 18, 2008

Black Mafia

wateka mtoto

Dar es Salaam


*Watoa masharti ya kupewa sh. milioni 10
*Baba mtu ajitosa msituni usiku kuwapelekea

Na Mwandishi Wetu

KUNDI la majambazi linalojiita Black Mafia, limemteka mtoto Fardosa Mohamed Othuman (miaka 2 pichani akiwa na mama yake Anab Ahmed), mwenye asili ya kisomali mkazi wa Mtoni Saba Saba, Dar es Salaam.

Tukio la kutekwa kwa mtoto huyo ambalo lilitokea juzi saa 3 asubuhi karibu na baa ya Ikweta Grill.

Akizungumzia tukio hilo Dar es Salaam jana, mama mzazi wa mtoto huyo, Bibi Anab Ahmed, alidai kuwa mtoto wake alitekwa saa tatu asubuhi, huku watekaji wakiacha masharti makali kwa familia yake.

Alidai kuwa masharti yaliyoachwa na watekaji hao ni kwamba hawatakiwi kutoa taarifa sehemu yoyote wala kituo chochote cha Polisi na wakibainika kufanya hivyo, mtoto waliyemteka atauawa.

"Ni tukio la kusikitisha katika familia yetu, kwani baada ya mtoto kuchukuliwa na watu hao, wakatuachia masharti makali yakiwamo ya kututaka tufiche siri kwa kutosema kwa mtu yeyote kupitia barua ambayo walikuwa wameleta saa chache kabla ya kumteka mtoto wangu," alidai Bibi Ahmed.

No comments: