'Kama
Na Mwandishi Wetu
HOJA ya Zanzibar kutambuliwa kama nchi ama la imezidi kuchukua sura mpya ambapo aliyekuwa mshauri wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour, Bw. Mohamed Raza, ameibuka na kupinga kauli zinazodai visiwa hivyo si nchi kamili.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Raza alisema historia inaonesha kuwa Zanzibar ni nchi inayotambulika duniani kwa zaidi ya miaka 1,000 na haiwezi kulinganishwa na Tanganyika iliyotambulika utaifa wake mwaka 1921.
Alitaja vigezo vinavyofanya Zanzibar kuwa nchi kamili kwamba ni pamoja na kuwa na Rais, Mahakama, Baraza la Wawakilishi na Serikali inayojitegemea.
"Unaposema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kilimanjaro, Tabora , Morogoro na mikoa mingine unaiweka wapi ?" Alihoji.
Bw. Raza ambaye ni mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema kwa mujibu wa protokali viongozi wa nje wanapotembekea Zanzibar, hupigiwa mizinga kama ishara ya heshima katika nchi yenye mamlaka kamili.
1 comment:
Mbona Mohammed Raza akipanua mdomo wake na kusema kitu hakuna wa kumjibu? Inaonyesha jamaa ana ubavu mzito ndani ya CCM.
Post a Comment