Sunday, July 20, 2008

Muafaka baada ya

uchaguzi haufai


20.07.2008 13:02:52
Na Mwandishi Wetu


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro (pichani) amesema utaratibu wa kutafuta muafaka baada ya uchaguzi mkuu, sio utamaduni unaopaswa kuendelezwa.

Badala yake amezitaka nchi za Afrika kujenga misingi imara ya demokrasia na kufanya chaguzi zilizo huru na haki ili kuepusha kupinga matokeo ya uchaguzi kunakosababisha kutumia muda mwingi na gharama kwenye mazungumzo ya usuluhishi wa migogoro inayotokea baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Dk. Asha-Rose ambaye yupo nchini kwa mapumziko, alitoa ushauri huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Alikuwa akijibu swali la mwanahabari aliyetaka kupata maoni ya UN iwapo inaunga mkono utamaduni unaoibuka sasa barani Afrika wa kukimbilia kutafuta muafaka baina ya wanasiasa wanaodaiwa kushindwa kwenye uchaguzi mkuu kwa njia ya hila na wapinzani wao.

``Huo sio utamaduni wa kuendelezwa, kinachotakiwa ni kujenga utaratibu wa kuwa na demokrasia na kuelimishana kijamii,`` alisema na kuongeza kuwa, ``dawa ni kujenga misingi imara ya demokrasia na baada ya uchaguzi, isiwe tena tunatumia muda mrefu kushughulikia matatizo yatokanayo na uchachguzi mkuu.``

No comments: