Mwili wa Marehemu
Mzee Mayagilo
Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa bendi ya brass ya polisi miaka ya nyuma mzee John Dotto Mayagilo (Pichani)ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya aga khan, jijini Dar es Salaam, umesafirishwa leo kuelekea kijijini kwake Matinde, Shinyanga,kwa mazishi.
Mzee Mayagilo atakumbukwa kwa umahiri wake katika muziki ambapo alikuwa kivutio pale alipoongoza brass band ama halaiki kwa mbwembwe zake ambazo zilimpatia sifa ndani na nje ya nchi.
Picha ya kwanza juu ni marehemu mzee mayagilo akiwa kitandani hospitali ya taifa ya Muhimbili mwaka jana alipoanza kuumwa na nyingine wakati akifanya vitu vyake katika bendi ya polisi. Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu,Thomas Mayagilo, Mzee Mayagilo amefariki akiwa na umri wa miaka 88 kwa kusumbuliwa na kuvuja damu kichwani, Presha na Stroke. Habari kwa msaada wa Mdau Michu.
*****
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA
PEPONI AMEN
Kwa hisani ya mdau
http://haki-hakingowi.blogspot.com/
Kwa hisani ya mdau
http://haki-hakingowi.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment