Sunday, July 20, 2008

Polisi kuendelea kumchunguza

Kubenea...Adaiwa kusambaza

akaunti za watu kwenye

mtandao...Wateja waijia

juu NBC, mfanyakazi

wake ahojiwa


IJUMAA 18, 2008, Tanzania kwa mara nyingine tena imeshuhudia uhuru wa habari ukiminywa na watawala. Gazeti hili la wananchi lilivamiwa na makachero na kufanya upekuzi kutokana na kile walichoita polisi, “kutafuta akaunti za siri za serikali na viongozi wake.”

Aidha, upekezi ulifanyika pia nyumbani kwa Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo, Saed Kubenea.

MwanaHALISI na wote wanaoipenda Tanzania wanalaani kwa nguvu zote uvamizi huo.

Makachero ndani ya ofisi ya MwanaHalisi
Makachero wakiondoka na kompyuta ya MwanaHalisi
Baadhi ya Makachero nje ya ofisi ya MwanaHalisi
Kachero akihojiwa na waandishi wa habari nje ya Ofisi za MwanaHalisi
Makachero wakiondoka baada ya kufanikisha azma yao

kutoka gazeti la MwanaHALISI la mtandaoni

No comments: