Monday, July 21, 2008


Razza aishangaa

CCM Bara



na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA maarufu visiwani Zanzibar, Mohammed Razza, amelalamikia msimamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bara kuwa Zanzibar si nchi.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Razza alisema msimamo huo ni mbaya na kamwe haukupaswa kutolewa na chama hicho Bara.

Kauli anayoilalamikia Razza ni ile iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha chama hicho taifa, Tambwe Hizza, kuwa Zanzibar si nchi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki huku akitumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar, Tambwe alisema suala hilo halina utata, kwani linaweza kuthibitishwa na sheria.

“Mimi kwanza nawashangaa sana wenzetu wa Bara kwa kumwacha Tambwe atangaze msimamo wa CCM Bara kwamba Zanzibar si nchi. Hii ni hatari kubwa. Zanzibar msimamo wetu wote, CUF na CCM, ndani ya Baraza la Wawakilishi na hata nje ya baraza ni kuwa Zanzibar ni nchi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na sasa kauli ya Tambwe, inasisitiza kuwa Zanzibar si nchi. Mvutano huu utatupeleka wapi?” alihoji Razza.


No comments: