Friday, July 25, 2008

Walimu 250 wa

Kiswahili wahitajika

Nigeria



JIBU LA SWALI LA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO

Mhe. Ludovick Mwananzila (CCM)

na Irene Mark, Dodoma

KWA miaka minne sasa, serikali inatafuta walimu 250 wenye sifa za kutosha kufundisha Kiswahili nchini Nigeria.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, alieleza hayo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kalambo, Ludovick Mwananzila (CCM), aliyetaka kujua iwapo serikali imekubali ombi la Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria kutaka walimu wa Kiswahili.

“Kwa kuwa imepita miaka minne sasa tangu Rais wa Nigeria, Obasanjo, alipoomba walimu 250 wa Kiswahili kwa ajili ya shule zake, serikali imefikia wapi hadi sasa?” aliuliza mbunge huyo.

Katika majibu yake, Bendera alisema bado serikali haijawapeleka walimu hao kwa sababu inaendelea kuwatafuta wenye sifa na uwezo wa kufundisha Kiswahili kwa ufasaha.

Aidha, alikiri kwamba serikali imepokea maombi ya walimu zaidi ya 1,000 wa Kiswahili katika nchi za Kongo, Libya na Nigeria na kwamba mchakato wa kuwapata walimu wazuri zaidi unaendelea.

No comments: