Kada CCM afanya kufuru,
atoa shs. Milioni 400,-
mkutano mkuu wa UVCCM
WAKATI kampeni za kuwania uongozi ndani ya Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeanza, mfanyabiashara maarufu ambaye ni mmiliki na mkurugenzi wa kampuni ya Shivacom, Tanil Somaiya, ametoa msaada wa sh milioni 400 kwa ajili ya kugharamia mkutano mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM).
Somaiya alitoa msaada huo jana mbele ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, katika hafla iliyofanyika katika jengo la Makao Makuu ya chama hicho la White House, mjini hapa.
Mbali ya fedha hizo, mfanyabiashara huyo alitoa pia fulana 1000, kofia 1000, mabegi 1,000 maalum kwa ajili ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi, vitabu vidogo 1,000 (Note Book) na bendera za UVCCM; vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni 250.
“Mimi ni mkereketwa na kada wa CCM, hivyo nimeamua kwa mapenzi yangu kutoa msaada huo kwa ajili ya kugharamia mkutano mkuu wa uchaguzi wa jumuiya hiyo,” alisema mfanyabiashara huyo, huku akiwashangaza wajumbe wengi wa NEC waliohudhuria hafla hiyo....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment