Saturday, November 15, 2008

Mwanafalsafa kuimba

na Akon 


Mwanafalsafa (kulia) akiwa na AY


na Shabani Matutu

MSANII wa kizazi kipya Khamis Mwinjuma  "Mwanafalsafa au "Mwana FA" anatarajia kuachia wimbo wake mpya akiwa amemshirikisha muimbaji mkali mwenye asili ya Afrika, Akon.

Mwana FA aliyabainisha hayo hivi karibuni mara baada ya kurejea nchini akitokea nchini Marekani.

Mwana FA amedai kwamba wimbo huo ambao anatarajia kuutengeneza na mkali huyo atautengeneza kipindi chake cha pili ambacho anatarajia kwenda hivi karibuni.

Pia Mwana FA alidai kwamba wakati atakaokuwepo hapa nyumbani ataachia video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Naongea na wewe’.

“Wimbo huo ni moja kati ya nyimbo ambazo zipo kwenye kazi yangu mpya ya albamu ya ‘Mabibi na mabwana’,” alisema. Mwana FA alibainisha kwamba albamu yake hiyo ameshaimaliza na taratibu zote zinazoihusu ameshazimaliza.


Bado Nipo Nipo



Angalia tovuti ya Mwanafalsafa: http://www.binamu13.com/


No comments: