Monday, April 27, 2009

Ze Utamu

wamekosa

adabu na heshima!



Jamani huu uhuru wa kutoa mawazo, kusoma, kupokea habari na kusema bila kuingiliwa na mamlaka za dola, una kikomo chake.

Zeutamu wamevuka kikomo kwa jinsi walivyobadili picha ya wanaume wawili wakifanya mapenzi na kuweka kichwa cha Rais wetu kana kwamba Rais ndiye ana….. na huyo mwanamme mwenzake, ni kukosa adabu na heshima kwa Rais wetu.

Kitendo walichofanya zeutamu, hakikubaliki kwenye mila, desturi na tamaduni za aina yeyote hapa duniani. Ni kitendo cha aibu na cha kupigiwa kelele kulaaniwa.

Hapa Norway, ambako kuna uhuru wa kusema unavyotaka, kuandika, kusoma habari unazotaka, kutoa maoni yako unavyotaka na ambako majarida ya picha za wanawake walio uchi yanauzwa kwenye vioski, bado watu hawafanyi ambayo yanayotokea nchini Tanzania kwa sasa.

Hapa Norway pamoja na yote hayo kuna kikomo chake cha huo uhuru. Kuna sheria ambazo zinaweza kukufanya upelekwe mahakamani na kushtakiwa kwa kuvuka kikomo cha uhuru wa habari.

Kwa mtu kukubali mwenyewe kwa ridhaa yake kuwekwa kwenye mtandao kama wa zeutamu au majarida au hata kwenye kideo, hilo sina tatizo nalo. Ni ridhaa ya mtu mzima na akili (kama ni mtu mzima na akili yake timamu).

Mimi ni mpigania haki za uhuru wa habari, kusema, kusoma ninachopenda, kuangalia, kupokea habari, lakini walichofanya zeutamu, si cha busara hata kidogo!!!

Hata kama mtu hapendi jinsi Rais Kikwete anavyoongoza nchi, au hampendi tu Rais Kikwete kwa hulka yake, kuna namna ya kuzifikisha hizo tofauti kwenye vyombo vya habari. Mbona kuna mengi tu yanaandikwa kuhusu Rais Kikwete au yanasemwa lakini hatuyapigii kelele? Ni kwa sababu yameandikwa kwa mantiki yanayokubalika kwenye jamii ya Watanzania.

Tamati ngoja niishie hapa, nisije nikapoteza lengo la kukasirishwa kwangu na yaliyofanywa na zeutamu…

 

Wenu Tausi Usi Ame Makame,

Oslo,  Norway.

tausi@online.no

No comments: