Saturday, May 16, 2009

Usalama wa taifa Norway

wagundua njama za kutaka

kufanya vitendo vya kigaidi.

Kati ya waliokamatwa ni

imamu aliyekuwa waziri wa afya

kwenye serikali ya Talibani

 

 

Idara ya Usalama wa taifa ya Norway, Politiets Sikkerhetstjenesten (PST), imewakamata vijana 25 wa Kiislamu wenye msimamo mkali wa kidini, kwa kupanga vitendo vya kigaidi nchini Norway. Hayo yalisemwa jana mjini Oslo na Mkurugenzi Mkuu wa PST, Bw. Jørn Holme.

Kufuatia maelezo ya Holme, vijana hao walishawishiwa na imamu wenye miaka 49 wa msikiti mmoja sehemu ya Grønland mjini Oslo, ambaye aliwahi kuwa waziri wa afya kwenye serikali ya Talibani nchini Afghanistan kati ya 1999 hadi 2001. Imamu huyo alikuja nchini Norway mwaka 2001 na kupewa hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa.

Kabla ya tukio hili la kupanga ugaidi, imamu huyo alikuwa anatafutiwa njia za kumwondoa nchini, baada ya kumpiga binti yake kwa kuwa na mawasiliano ya barua pepe na kijana mmoja wa Kihindi. Kwa vile hairuhusiwi kupiga mtoto hapa Norway, jamaa alipelekwa mahakamani na kesi yake ilisikilizwa kati ya Mei na Septemba mwaka jana na alikuhukumiwa kifungo cha miezi minne.

Bw. Holme alisema kuwa vijana wake walianza kumfuatilia huyo imamu na vijana aliokuwa anawashawishi kwa kusikiliza simu zao, kusoma barua pepe zao na kusikiliza mahubiri makali ya huyo imamu kwenye msikiti wake na kila walipokuwa wanapiga hatua na baadaye vijana wake wakawafuata hao vijana na huyo imamu walipoenda Peshawar nchini Pakistani kupewa mafunzo ya kigaidi.

Baada ya kurudi, watoto wa kazi wa PST, waliwafuata majumbani kwao, wote waliokuwa wanawashuku na kuwatonya kuwa wameshawagundua nini wanataka kufanya. Baada ya muda wakawakamata wote kwa mpigo na kuwaweka lupango.Baadhi yao wameshafukuzwa nchini, Bw. Holme alikataa kutoa idadi ya waliofukuzwa.

No comments: