Brazil yawachezea Uruguay
nyumbani kwao 4 – 0.
Hawajawahi kuwafunga
kwao kwa miaka 33 !!!!
Jana Jumamosi mjini Montevideo Uruguay, Brazil wamewachezea Uruguay kwa kuwafunga magoli 4 kwa bila. Brazil hawajawahi kuwafunga Uruguay nyumbani kwao kwa miaka 33. Hiyo inawafanya Brazil kuongoza kundi la Amerika Kusini kwenye michezo ya kuwania kucheza fainali za kombe la dunia mwakani nchini Afrika Kusini. Goli la kwanza la Brazil lilifungwa na Daniel Alves kwenye dakika ya 12 tu toka mechi kuanza. Kabla ya mapumziko, Juan aliipatia Brazil goli la pili.
Dakika saba ya kipindi cha pili, Luis Fabio alifunga goli la tatu na la nne lilifungwa na Kaka (ambaye amefaulu uchunguzi wa daktari wa kuichezea Real Madrid msimu ujao) robo saa kabla ya mpira kwisha. Kwenye kundi hilo, Argentina waliwaza Colombia goli 1 kwa sifuri, Venezuela vs. Bolivia 1 – 0 na Chile wameifunga Paraguay 2 – 0. Brazil inaongoza kundi hilo kwa pointi 24, Paraguay nayo ina pointi 24. Brazil inaongoza kwa tofauti ya magoli. Imefunga magoli 23 na kufungwa 5, Paraguay wamefunga magoli 19 na kufungwa 11.
No comments:
Post a Comment