Je una wasiwasi kuwa
Umeibiwa habari binafsi?
Jana wizara ya sheria na polisi ikishirikiana na NorSIS(Norwegian Center for Information and Security) na Norwegian data inspectorate (datatilysnet), wamezindua tovuti ya kuwafahamisha wananchi juu ya wizi wa habari binafsi za wananchi. Wizi wa namna hii, umekuwa ukizidi kila kukicha hapa Norway na kwingine duniani:
Wanorwejiani wengi wamekuwa wakiibiwa vitambulisho vya benki na pasipoti. Wengi wamejikuta na malundo ya madeni baadaya ya kuibiwa habari zao binafsi. Wezi wamekuwa wakinunua vitu vya gharama kubwa kama magari, simu za viganja za bei mbaya, vito vya thamani, kufungua akaunti mpya za benki, kuagiza kadi mpya za benki, kuchukulia mikopo toka benki, na vitu vinavyofanana na namna hiyo. Wezi wengine wamewahi hata kuombea pasipoti kwa habari binafsi zisizo zao! Gharama zote huwarudia watu waliopoteza ”Identity” zao. Kuwa mwangalifu, majira ya Kiangazi yameanza na ndiyo majira ya watu wengu kuibiwa au kupoteza vitambulisho na pasipoti. Endapo utagundua umeibiwa, toa taarifa haraka kituo cha polisi.
No comments:
Post a Comment