Sunday, June 21, 2009

Mmiliki wa ZeUtamu

akamatwa


Hii habari kidogo ina utata. Kama kweli Bw. Lusinde ni raia wa Uingereza, na kwa kuwa Tanzania haina uduo, basi ubalozi wa Tanzania hapo Uingereza unahusika vipi na mtu ambaye si Mtanzania? Hii inashangaza zaidi ukizingatia kwamba ubalozi wa Tanzania uliopo Marekani mpaka sasa umeshindwa kujihusisha hata kidogo na mshitakiwa Ahmed Ghailani, ambaye uraia wake wa Tanzania hauna utata, na ambaye anakabiliwa na mashitaka mazito ambayo yakithibitika huenda akaishia kupewa adhabu ya kifo.

Katika mazingira ambayo mgeni anakabiliwa na kesi ya ugaidi na mauaji dhidi ya wamarekani, katika mahakama ya Marekani, kuna sababu ya kutia shaka iwapo haki kweli itatatendeka bila usimamizi makini. Kazi ya ubalozi ni pamoja na kuhakikisha haki inatendeka na Mtanzania anapewa uwezo wa kujitetea, maana kushitakiwa pekee hakumaanishi kwamba mtuhumiwa kweli ana hatia.

Lakini sasa tunaona vipaumbele vya serikali-wezi wa mabilioni wanapeta, mTanzania ambaye maisha yake yako hatarini hapewi ushirikiano wa balozi wake, kana vile wana uhakika na hatia yake, lakini masuala ya nguoni yanayowavunjia "hadhi" wakuu-haraka sana yanashughulikiwa. Bila shaka muda, na pesa nyingi (posho n.k) vimetumika ili kumpata na kumrejesha Lusinde Tanzania.

Kutoka Tanzanet. Mwandishi: Jina kapuni.

No comments: