PROFESA HAROUB
OTHMAN AFARIKI LEO
PROFESA HAROUB OTHMAN, MMOJA WA WAHADHIRI WAANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI HII HUKO UNGUJA AKIWA USINGIZINI.
MWANA WA MAREHEMU, TAHIR OTHMA, AKITHIBITISHA HABARI HII AKIWA NJIANI KUELEKEA MSIBANI AKITOKEA DAR, AMEIAMBIA GLOBU YA JAMII KWAMBA MAREHEMU AMEKUTWA AMEFARIKI ASUBUHI HII AMBAPO JANA ALILALA AKIWA BUHERI WA AFYA.
HABARI TOKA UNGUJA ZINASEMA MAREHEMU PROFESA HAROUB OTHMAN USIKU WA KUAMKIA LEO ALIHUDHURIA UZINDUZI WA TAMASHA LA MAJAHAZI (ZIFF) KATIKA NGOME KONGWE NA HAKUONEKANA NA MATATIZO YOYOTE KIAFYA.
MSIBA UKO NYUMBANI KWAKE SEHEMU ZA MICHENZANI ENEO LA BARASTE, NA HAIJAJULIKANA KAMA ATAZIKWA LINI. HABARI ZA MAZISHI YAKE TUTAWALETE MARA ZITAPOPATIKANA.
PROFESA OTHMAN, ALIYEKUWA MHADHIRI WA DEVELOPMENT STUDIES HAPO UDSM, AMEANDIKA SANA MASUALA YA MAENDELEO YA AFRIKA NA ALIKUWA MSEMAJI ANAYEHESHIMIKA KUHUSU MASUALA YA BARA LA AFRIKA NA AGHALABU VYOMBO VYA HABARI VYA NYUMBANI NA VYA KIMATAIFA VILIKUWA KILA MARA VIKIMHOJI KILA LITOKEAPO JAMBO KUBWA LINALOHUSU BARA HILI.
ATAKUMBUKWA PIA KWA UCHAMBUZI WAKE WA MAMBO YA HALI YA KISIASA SEHEMU MBALIMBALI BARANI AFRIKA NA ULIMWENGU KWA JUMLA, MOJAWAPO IKIWA NI MADA NYETI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR PAMOJA NA MIGOGORO YA SOMALIA NA DARFUR. SOMA BAADHI YA MAANDIKO YAKE KUHUSU MUUNGANO:
bofya hapa
GLOBU YA JAMII INATOA POLE KWA WAFIWA NA KUMUOMBA MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
-AMIN
Kwa Hisani ya Muhidin Issa Michuzi
No comments:
Post a Comment