Wezi wa pin-code
watumia darubini!!!
Jamaa mmoja, Kim Halvor Hartvik alikuwa Stesheni Kuu ya Treni mjini Oslo asubuhi ya leo. Akaenda kwenye ATM (Automatic Teller Machine) kuchukua hela, jamaa kwa uangalifu akaangalia kulia na kushoto, nyuma na mbele hakuona mtu karibu. Akagonga nywila (pin code) na kuchukua hela, akasubiri treni ya anakokwenda mjini wa Moss, mashariki ya Norway. Treni ikaja, wakati akiwa mlangoni kuingia, akaona msongamano usio wa lazima. Ghafla bin vuu, kushtuka hana pochi.
Jamaa akachukua simu yake ya kiganja na kupiga kwenye benki yake wakafunga akaunti. Hii ya jamaa kushtuka kuibiwa pochi yake na kupiga simu kwenye benki yake na polisi haikuchukua hata dakika 3.
Kwenye hizo dakika 3, wezi walifanikiwa kuchukua kroner 17.000,- (kumi na saba elfu). Kapteni Inge Sundeng, wa kituo cha polisi cha Grønland, amethibitisha kuwa wezi wa nywila (pin code) huwa wanakaa mbali na darubini kuangalia namba siri za mwibiwa mlengwa halafu wanatumiana hizo nywila kwenye SMS na kupanga mikakati ya kumwibia mlengwa.
No comments:
Post a Comment