Friday, July 31, 2009


Duh! mbavu ziliwauma!

Walokole walikuwa wanapita mtaani, ghafla wakamkuta mlevi mtaroni kajilaza utadhani yuko kwake. Wakaanza kumwombea, alipozinduka wakamuuliza, je wamjua YESU? Mlevi akajibu hataa! mimi ni mgeni mtaa huu!.


Aliyepanda treni siyo msafiri

Wadada wawili katika Jiji la Mbeya walikwenda stesheni ya treni kwa lengo la kusafiri, walipofika wakakuta treni inaondoka, wakaikimbiza, mmoja akapanda mwingine akashindwa na kubaki akicheka, watu wakabaki wakimshangaa na kumuuliza unacheka nini? Akajibu: Aliyepanda alikuwa ananisindikiza tu, mimi ndiye ninayesafiri.


Wanasiasa wazikwa hai

Ilikuwa ajali ya basi lilikuwa limejaza wanasiasa ambalo liliacha njia na kugonga mti katika shamba la mkulima. Baada ya mkulima huyo kuliona gari hilo, alisogelea eneo la tukio kuona nini kilitokea, alipowaona majeruhi wa ajali hiyo, alifanya kile alichostahili kufanya kwa nafasi yake. Siku chache baadaye, walifika polisi waliokuwa wamepata taarifa za kutokea kwa ajali, walimuuliza mkulima wako wapi wanasiasa waliopata ajali.


MKULIMA: Niliwafukia wote!

POLISI: Kwani walikufa?

MKULIMA: Baadhi yao waliniambia hawajafa lakini si unajua uongo wwao? Mimi nilifanya hivyo kwani walinidanganya kuwa hawajafa!A

Kutoka Global Publishers


No comments: