Monday, July 20, 2009

Miaka 40 ya Apollo 11

kutua mwezini


Kutoka kushoto: Neil Amstrong, Michael Collins na Edwin E. "Buzz" Aldrin


Lunar Module "The Eagle"


Saa 20:17:40 UTC (Marekani) tarehe 20. Julai 1969, chombo cha kwanza kilichokuwa kikiendeshwa na binadamu toka duniani "Lunar Module au Eagle (Apollo 11)" kilitua mwezini. Baada ya kutua kamanda Neil Amstrong aliwaambia wataalamu na waongozaji wa Apollo 11 waliokuwa Kennedy Space Center, Houston:

"Houston, Tranqulity Base here. The Eagle has landed"

Na waongozaji wa Apollo waliokuwa Kennedy Space Center walimjibu:

"Roger, Tranquility. We copy you on the ground. You got a lot of guys about to turn blue. Thanks a lot"

Saa 02:56 EDT (Marekani) tarehe 21. Julai 1969, binadamu wa kwanza alikanyaga mwezini na alikuwa kamanda Neil Amstrong na alisema msemo maarufu:

"That´s small step for a man, one giant leap for mankind"

Amstrong alifuatiwa na binadamu wa pili kukanyaga mwezi, kamanda Edwin Eugene "Buzz" Aldrin; huku mwenzao, kamanda Michael Collins akivinjari angani na kuwasubiri Amstrong na Buzz Aldrin.

Apollo 11 ilirushwa angani saa 13:32 UTC (Marekani), tarehe 16. Julai 1969 kutokea Kennedy Space Center, Houston.

Misheni hii ilikuwa hitimisho la hotuba ya Rais John F. Kennedy, aliyoitoa kwenye mkusanyiko wa Bunge la Marekani; Congress tarehe 25. Mei 1961 aliposema:

"I believe that this nation should commit itself to achieving the goal, before this decade is out, of landing a man on the Moon and returning him safely to the Earth:"



No comments: