Kuala Lumpur (Malaysia): Mlimbwende wa zamani na nesi, Bi.Kartika Sari Dewi Shukarno, amenusurika kuchapwaviboko sita na faini ya Ringgit5000,- (kroner 9000,- /T.shs. 1 946 430,93).Binti huyo alivunja sheria ya Kiislam kwa kunywa pombe kwenye baa moja mwaka jana.
Bi. Kartika alikubali mahakamani kuwa alikunywa pombe na atakubali hukumu yoyote atakayopewa. Amelipa faini na alikuwa anasubiri kuchapwa viboko.
Serikali ya Malaysia imeingilia kati, baada ya kesi kujulikana duniani na kuamua kumwachilia binti huyo bila kuchapwa viboko.
Kuna sheria na mahakama za aina mbili nchini Malaysia, moja ni sheria na mahakama za kawaida na nyingine ni mahakama ya kadhi, ambayo ndiyo iliyomhukumu huyo binti kwa sheria za Kiislam.
Watu wengine kama Wachina na Wahindi wao sheria za mahakama ya kadhi haziwahusu, hivyo wanaruhusiwa kunywa na kufanya starehe bila kuguswa na mahakama ya kadhi.
No comments:
Post a Comment