Wakazi wa kijiji wachoshwa
Na watu wanaofanya ngono
kwenye kijiji chao kiitwacho
“Fucking”
Kibao kinanyoonyesha kuwa sasa unaingia kijiji cha "Fucking"
Wakazi wa kijiji kimoja kiitwacho “Fucking” nchini Austria wamechoshwa na watu wanaoendesha hapo kwenye hicho kibao na kufanya ngono. Uvumi umekuwa ukizidi kuenea kuhusu kijiji hicho, na watu na watalii wamekuwa wakitalii sehemu hiyo, wakichukua picha au hata “kufanya shughuli za kiutuuzima” kwenye kibao hicho. Kijiji hicho kipo tangu mwaka 1070. Kilipewa jina la “Focko” la mtu mmoja maarufu aliyekuwa akikaa hapo. “Ing” imetokana na lugha ya Kijerumani, ikiwa na maana “Familia ya” na ikapatika “Fucking” ikiwa na maana “Familia ya Focko”. Wakazi wa kijiji wameamua kuweka kamera za CCTV.
No comments:
Post a Comment