Tuesday, August 11, 2009

Onyo kwa wabakaji: Yaliyotokea Norway


Jamaa abaka na kuukwa

UKIMWI



Jamaa mmoja ambaka dada mmoja na kuukwaa UKIMWI. Hiyo siku huyo jamaa alipoamua kufanya unyama huo, alimfuata huyo dada huyo kwa kumvizia vizia toka klabu moja. Alipofika kwenye kona moja hivi, jamaa akamkamata dada watu. Kabla jamaa hajaanza kufanya uchafu wake, huyo dada alimwomba jamaa avae kondom. Jamaa hakusikiliza. Jamaa akafanya shughuli zake. Jamaa akakamatwa na polisi baada ya siku chache. Jamaa akafunguliwa mashtaka. Wakiwa mahakamani, jamaa akaambiwa kuwa sababu ya huyo dada kumwambia avae kondom ile siku aliyobaka, ni kuwa huyo dada alikuwa anamwonea huruma na alishindwa kumwambia kuwa ana VVU (Virusi Vya Ukimwi). Jamaa amelazimishwa kupimwa na mahakama na amegundulika kuwa kaambukizwa.

4 comments:

Anonymous said...

Mna uhakika gani kuwa ndiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kubaka? Kama alikuwa natabia hiyo tangu zamani inawezekana naye alikuwa na ukimwi kabla hajambaka huyo dada.

Kusema dada huyo alimwonea huruma na kumwomba avae condom yaani ana huruma kuliko baba mtakatifu? Kwanini hakumwambia wazi kwamba alikuwa na ukimwai hili aepukane na kitendo cha kubakwa.

Hii story siiamini.

Mhariri wa blogu said...

Hii story iko mahakamani hapa Oslo, Norway. Si ya kubuni. Amini usiamini ni ya kweli.

Jamaa wamecheki DNA yake na kesi zingine za kubaka wamekuta ndiyo ya kwanza ya kubaka.

Anonymous said...

Kama alivyosema huyo wa kwanza hii story haiamini, hata mimi siamini hivi kweli mtu anataka kunibaka halafu nimwonee huruma? Eti nimwambie tafadhali uvae condom? wakati amejitakia kifo!

Labda mtu atakae nitongoza huyo ndo nitamwambia vizuri hali yangu nilonayo ila sio m bakaji acha nae ajipake ududu tufe wote.

Sina huruma na wabakaji acha nae ajutie ubakaji wake tena akome kumjua huyo dada.

Mhariri said...

Hiyo kesi kama nilivyotangulia kuwa iko mahakamani. Huo ni ushahidi wa mwanamke aliyebakwa. Sasa sijui alisema hivyo ili aachiwe akimbie au ilikuwaje...haikusemwa mahakamani.

Nitawaleleza zaidi jinsi kesi inavyoendelea...bado hukumu haijatolewa.

KAENI CHONJO!