Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa waumini wa dini ya kiislamu Tanzania na wale wasio waislamu siku ya jana baada ya kuzinduliwa kwa Muongozo wa Waislamu wenye lengo la kupigania haki yao katika masuala mbalimbali yakiwemo ya Kisiasa, kiuchumi, kidini na kimaendeleo.Hafla kubwa ya uzinduzi huo ilirindima katika viwanja vya Mnazi mmoja katikati ya jiji la Dar es Salaam ambapo Sheik Ponda Issa Ponda ndiye aliyezindua kitabu cha muongozo huo.Kwa sauti moja waislamu waliazimia kuwa katika uchaguzi mkuu 2010 watachagua kiongozi atakaye jali maslahi ya waislamu na taifa zima la Tanzania na kwamba wamechoka na hali yao duni ya maisha, huku wakichombeza kwa kibwagizo cha ‘2010 Hatudanganyiiiiiiiiiki” Uzinduzi wa Muongozo huo unakuja siku chache baada ya waumini wa kanisa Katoliki nchini kuzindua Waraka wao unaotoa msimamo wao katika uchaguzi Mkuu wa 2010.Yafuatayo ni matukio ya hafla hiyo katika picha.
Kutoka Global Publishers Tanzania
4 comments:
Leo hii kwa kuwa hao jamaa nao wameamua kutoa mtazamo wao ndio sasa suala limegeuka kuwa la udini? Kwani Kingunge alipokuwa anasema hamkufahamu nini alikusudia? Nyote mlikuwa ni watumwa wa fikra za dini yenu huku mkimkashifu. Sasa kaeni kimya ili udini uzidi kushika hatamu. Ingawa Kingunge yeye ni Atheist lakini ni dhahiri kuwa alichokuwa anakisema ni cha uhakika, kwamba nchi itaangamia kwa maoni ya kisiasa kama haya yanayotoka kwenye dini zetu!!!!! Acha sasa tuumie.
Mambo yote haya yanatokea Rais wetu Mtukufu kakaa kimya tuuu!!! Hasemi lolote!
Au yale yale ya funika kombe mwanaharamu apite!
MWENYEZI MUNGU ATUPISHE MBALI...NCHI INAANGAAMIA TARATIBU HUKU TUNAIONA BILA KUFANYA LOLOTE!!! RAIS KIKWETE NDIYE HUYO KIMYAAAA!!!! SITTA, KILANGO NA WENGINE WAKIPIGA KELELE, WANASULUBIWA!!!!
TWAFAAAAA!!!!!!!
Mchezo mdogo tu...serikali nayo itoe mwongozo wake kuhusu jumuiya za kidini...halafu tusikie hizo jumuiya zitasema nini?
Kwenye demokrasia ya kweli, watu wana uhuru wa kusema, kuandika,. n.k. bila kusulubiwa na serikali.
Kama jumuiya za kidini hazijavunja sheria na katiba ya nchi, waachiwe waandike wanavyotaka!
Post a Comment