Friday, September 18, 2009



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.

MPENZI Frank,

Vipi hali yako? Ni matumaini yangu u mzima si wazimu wa kunifikiria vingine tena. Sijui kwa nini unakuwa na imani ndogo hivyo kila nikisafiri mpenzi.

Jamani, mimi nifanye nini? Niko kazini Mama Bosi akinilazimisha nimsindikize wakati anaenda kwenye jimbo la bosi, mimi nifanye nini? Vibaya hivyo mpenzi. Wanifanya nikae roho juu kila wakati hadi nashindwa kufanya kazi. Juzi, baada ya kudondosha vikombe vitano huku nikiwazia wasiwasi wako, hata MB alitambua kwamba kuna shida, akaanza kuniuliza kulikoni na niliposhindwa kumridhisha akatishia kunifukuza kazi eti nimekuwa mzembe siku hizi.

Bofya na endelea>>>>>


No comments: