Thursday, September 17, 2009

Mambo kutoka kwa

dada Dina Marios



…….Mimi ni kijana 30 niko naishi na MPENZI wangu ambaye ndiye nitakaye mwita mama watoto wangu na sasa ana mimba ya miezi 4 na nusu juzi tarehe 13 alienda kliniki akapimwa vipimo vyote akaambiwa yeye tayari anayo VVU (Virusi Vya Ukimwi) nimeogopa moyoni nimeumia sana.Kesho yake na mimi nikaenda kupima mimi niko poa nikamshauri na yeye akapime tena hospitali nyingine akaambiwa yupo poa,ila mpaka sasa mi sina hamu ya kufanya naye ngono naogopa kwani najiuliza inamaana vile vipimo mara nyingine zinakosea au inakuaje? kiukweli sielewi

Naombeni mnishauri kwani mimi kwa sasa sina mzuka wa kufanya naye mapenzi kwani naogopa sana vvu naamini kwa ushauri wenu mimi nitasaidika na maisha kuendelea kazi njema kwenu.

Kutoka kwa dada Dina Marios

1 comment:

Anonymous said...

Nendeni wote kapimeni tena sehemu nyengine kabisa kila mmoja peke yake.