Tuesday, September 15, 2009

Matokeo ya uchaguzi mkuu

Norway



Jens Stoltenberg kuendelea kuongoza

baada ya uchaguzi Jumatatu 14.09.2009













Matokeo ya uchaguzi mkuu hapa Norway mpaka kwenye saa saba na nusu za usiku kuamkia Jumanne 15.09.2009, na asilimia 99% ya kura kuhesabiwa, yanaonyesha kuwa serikali ya mseto wa wekundu na kijani (rød-gønnregjering) wa Labour Party (Arbeiderpartiet kifupi AP), The Agrarian Party (Senterpartiet kifupi SP) na Socialist Left (Sosialistisk Vestreparti kifupi SV) umepata jumla ya wabunge 86, hivyo basi kuwa na wingi wa kura kuweza kuendelea kwa kipindi cha 2009 hadi 2013.

Upande wa kulia wa siasa hapa Norway, yaani Conservative (Høyre kifupi H), The Progress Party (Fremskrittspartiet kifupi FrP), Christian Democratic Party (Kristelig Folkepartiet kifupi KrF) na Liberal (Ventre kifupi V) jumla umepata jumla ya wabunge 83, hivyo basi kukosa wingi wa kura wa kuiangusha serikali ya mseto ya AP + SP + SV.

Vyama ambavyo vimefanya vibaya kwenye uchaguzi huu ni Venstre, kwani kiongozi wao Lars Sponheim, ameshindwa nafasi ya ubunge, hivyo kutangaza kujiuzulu nafasi uongozi wa chama hicho. Kingine ni KrF amabacho kimepata wabunge pungufu wa wabunge kutoka uchaguzi wa 2005. Vyama vingine ambavyo vimepata chini ya asilimia 4%, havitapata nafasi ya kuwakilishwa bungeni.

Idadi ya wabunge kwa kila chama:

Vyama vinavyounda serikali ya mseto

Arbeiderpartiet = wabunge 64

SV = wabunge 11

SP = wabunge 11

Jumla = wabunge 86

Vyama vya upinzani

Fremskrittspartiet = wabunge 40

Høyre (Hoeyre) = wabunge 31

Kristelig Folkeparti = wabunge 10

Venstre = wabunge 2

Jumla = wabunge 83

No comments: