Moja katika jimbo lililosahuliwa Tanzania ni jimbo la Tumbatu. Leo hii limekumbukwa kutokana na hilo daftari la kupiga kura. Huko wanaishi watu wa asili na jadi yaani Watumbatu. Huduma za afya, shule na ajira ziko taabani sana.
Sijui huyo Mbunge anaepigiwa Kura anawakilisha nani kwani huo mgao wa kila jimbo katika bajeti sidhani kama unafika. Watumbatu waliowahi kuona Professional College ni wachache mno. Huko VETA haikufika angalau watu wakapata ujuzi wa uvuvi wa kisasa na ufundi wa boti za kisasa. Kuna elimu kubwa ya jadi ya kuvinjari baharini ambayo watu hurithi kwa kufunzwa na wazee wao.Wakazi wa huko ni wavuvi na wakulima.
Kihistoria walikuwa wanafika bahari za mbali hadi India kwa kutumia majahazi ya jadi. Ni watu waliokuwa na viungo vya historia kuanzia hapo hadi Comoro, Philipiness, Yemeni. Kiongozi wa mwisho wa mamwinyi wa jadi yaani kabla ya usultani kutuwa Zanzibar, alikuwa ni imam alietokea kwa kizazi chake Philipines na kuchanga damu na watu wa kustawi hapo.
Amur
No comments:
Post a Comment