Wednesday, September 09, 2009

Shanga za miguu ”vikuku”




KUNA mdau kamtumia mdau wa Simulizi hiyo picha anauliza hizo shanga za miguuni zinavaliwa kujiremba au zina maana nyingine?

Kwa mujibu wa maelezo yake, amewahi kusikia kwamba, shanga hizo a.k.a vikuku zina maana yake hivyo anaomba kufahamu kama ni kweli.

Anasema, kaelezwa kwamba, kikuku kikivaliwa mguu wa kulia ina maana yake, na kikivaliwa kushoto kinakuwa na maana nyingine, ni kweli?

Kama kila mguu una maana yake, vikivaliwa miguu yote inamaanisha nini?

Soma zaidi kwenye blogu ya Simulizi


4 comments:

Tausi Usi Ame Makane, Oslo, Norway said...

Jamani duniani hakuna dogo! Mbona hizi shanga za miguu zimekuwa zikivaliwa na baadhi ya makabila, jamii za Kiafrika, baadhi ya jamii na makabila ya Asia, Wahindi wa Amerika, na hata Papua New Guinea?

Wamarekani ndio wametuiga.

Hiyo tafsiri iliyotolewa na Miss Angela kwenye:

http://simulizi.blogspot.com/2009/09/vikuku-ni-urembo-au.html#comment-form

naona imetungwa tu kwenda na tamaduni mpya



Je, watu watasema nini kuhusu vishaufu (vipini vya puani)?

Mama yangu alikuwa anavaa alipokuwa kijana. Enzi hizo za enzi.

Tusisahau kuwa Wazungu na Wamarekani

Tausi Usi Ame Makane, Oslo, Norway said...

..........................................................................

Tusisahau kuwa Wazungu na Wamarekani wameiga mengi kutoka kwetu...

Tausi Usi Ame Makame said...

Ni Tausi Usi Ame Makame siyo Makane. Vidole viliniponyoka....

Anonymous said...

Da´Tausi umenena,

Kuna wengine wanasema kuwa mwanamke anayevaa kikuku mguu wa kushoto ni msagaji na anayevaa miguu yote anatembea na wanaume na wanawake. Sijui wa kulia wanasemaje hawa wanaosema hivi.