Tuesday, September 08, 2009

Wanorweji wawili wahukumiwa

kuuawa nchini Kongo



Tjostolv Moland (28, t.v.) na Joshua French (27), wakisubiri hukumu yao leo asubuhi mjini Kisangani, Kongo.


Oslo (Norway): Vijana wawili wa Kinorwejiani; Tjostolv Moland (28) na Joshua French (27) wamehukumiwa na mahakama ya kijeshi mjini Kisangani kwa kuuawa mara tano leo hii. Vijana hao wawili wamehukumiwa kwa kutuhimiwa kumwua kijana mmoja Mkongo, Abedi Kasongo. Serikali ya Norway imehukumiwa kuilipa Kongo Dala za Kimarekani milioni 60. Moland na French wamehukumiwa kwa pamoja kumlipa mjane wa Abedi Kasongo Dala za Kimarekani 171,000.-

Wamehukumiwa kwa kutaka kuua, kuua, ujambazi kwa kutumia silaha, kukutwa na silaha bila idhini na kufanya ujasusi. Waziri wa mambo y a nchi za nje wa Norway, Jonas Gahr Stoere amekanusha vikali kuwa vijana hao wametumwa na serikali kufanya ujasusi nchini Kongo.

Moland na French walikodisha gari ya Abedi kutoka Kisangani na walipofika maporini, wakamwua na kutoroka. Walisakwa na wanajeshi wa Kongo kwa karibu wiki nzima na kukamatwa. Walipokamatwa, walikutwa na vitambulisho vya jeshi la Norway na pasipoti za bandia, ramani za kijeshi na GPS.

Moland na French wana siku 5 za kukata rufaa ya hukumu hiyo.

Moland na French waliwahi kuwa wanajeshi kwenye jeshi la Norway, pia wamewahi kuwa askari mamluki na walikuwa kwenye taratibu za kuanzisha kampuni ya ulinzi nchini Uganda.

Idara ya Usalama ya jeshi la Uganda; Chieftaincy of Military Intelligence (CMI), inadai Moland na French wanatafutwa nchini Uganda. CMI wamekamata bunduki, GSP, buti za kijeshi, nguo za kijeshi na visu kwenye nyumba waliyopanga mjini Kampala. CMI wanadai vijana hao walitaka kuanzisha SIG Uganda (kampuni binafsi ya ulinzi) kama ”cover” ya shughuli zao halisi za kimamluki.

Habari za hukumu hii ya kifo zimesambaa kwenye vyombo vya habari duniani:

Al Jazeera

BBC

CNN

Daily Nation (Kenya)

Vinginevyo

No comments: