Monday, October 05, 2009

Berlusconi achoshwa na

wageni wanaoishi Italia

bila makaratasi



Waziri mkuu wa Italia; Berlusconi.


Waziri mkuu wa Italia; Sylvio Berlusconi amechoshwa na wageni kibao waliojazana nchini Italia na ambao wanaishi bila vibali vya kuishi au kufanya kazi. Serikali yake imeamua kuwaweka ndani kwa ulinzi mkali wageni wote watakaokamatwa wanaoishi isivyo halali nchini humo. Serikali hiyo pia imeamua kutumia jeshi la Italia kuwadhibiti wageni wasio na makaratasi.

”Jela” moja kubwa ya kuwazuia wageni wasio na makaratasi iko Ponte Galeria nje kidogo ya mjini wa Roma. Kizuizi hicho kimezingirwa na wigo mkubwa wa seng´enge na unaolindwa na wanajeshi wakiwa na ma´mbwa. Baba Mtakatifu, asasi zisizo za kiserikali zinazotetea haki za binadamu na Umoja wa Mataifa unalaani kitendo hicho cha kuwafungia ”jela” wageni kana kwamba ni wahalifu. Serikali ya Italia inajitetea kwa kusema,; kuwa watu wengi wamezidi kuingia nchini humo isivyo halali na hiyo ndiyo njia pekee ya kudhibiti wageni kuingia kiholela na wanawekwa kwenye vizuizi na siyo jela.

Berlusconi anasema Italia si nchi ya kibaguzi; ila wanataka kuhakikisha kuwa wageni wanaoingia Italia ni watu wema na si wahalifu.

Kundi kubwa la wageni wanaoishi bila makatasi nchini Italia:

1. Waromania 625 000

2. Waalbania 402 000

3. Wamoroko 366 000

4. Wachina 157 000

5. Waukraina 133 000

6. Wafilipino 106 00

7. Watunisia 94 000

Chanzo: Caritas, Istat


No comments: