Thursday, October 01, 2009

Mambo kutoka kwa dada Dina Marios...

Kuna wakati lazima uachane

na marafiki ambao kiukweli

wanakuumiza kiafya...



Kiukweli si kila rafiki katika maisha yetu ni mzuri kwetu na anatutakia mema. Maadui zetu wakubwa ni marafiki zetu, mtu wa mbali hawezi kukutendea uovu kukudhuru wakati hajui pa kuanzia lakini marafiki zetu ndio hutumaliza kwa sababu wengi wanatujua vyema nguvu na mapungufu yetu.

Mimi kuna shost mmoja kaniudhi sana kiasi kwamba sitaki kumuona wala kumsikia huyu bidada amekuwa na tabia kwa takribani miaka miwili anatumia namba tofauti kujifanya watu tofauti wanaotaka kuwasiliana na mimi.

Mara kadhaa amejifanya mwanaume anayenitongoza kunitaka kimapenzi, mara kadhaa amejifanya mwanamke wale maaraufu (wasagaji) akinitaka kimapenzi...kama haitoshi hujifanya ni miongoni mwa maadui zangu na kuanza kunitumia meseji za matusi kunitukana tena matusi ya nguoni...kwa kipindi chote nilikuwa namuhisi ila sikuwa na uhakika lakini kama ujuavyo za mwizi arobaini ile Jumamosi kuamkia Idd akanitusi sana kwa namba ambayo ninayo nimeisave toka miaka miwili iliyopita..

Kwanza alinitext kwa namba yake ninayoijua kunialika Idd kwa sababu nilikuwa shopping sikuweza kujibu ujumbe wake...baada ya dk 2 zikaanza kuingia msg za matusi mfululizo akinitusi mimi, kazi yangu, blog yangu akaitusii pia na hata maisha yangu kwa ujumla...unajua ni kiasi gani inauma mtu kukudhalilisha na kukushusha utu wako.Ila mimi nikamjua na nikasema its time kumfahamisha kuwa namjua kwa muda tu na huo mchezo wake....kweli akakubali..eti anajitetea alikuwa akinipima....jamani kwa miaka miwili unanipima??

unanipima kitu gani kwa mfano wewe ni mungu?nikamwmbia kwa wema tu she dont deserve to be my friend,she is a very good person but hafai kuwa rafiki yangu coz she is a snake.

Toka that day amekuwa akituma msg za kuomba samahani,nikamwambia nimemsamehe but hatuwezi kuwa marafiki maana nahitaji marafiki wakweli katika maisha yangu wale watakaokuwepo nami na kusimama nami na si kushiriki kuniumiza.

Bofya na soma maoni ya wasomaji kwenye blogu ya dada Dina Marios

NOTE.

Making a million friends is not a miracle,the miracle is to make a friend who will stand by you when millions are against you.

Kwa idhini ya dada Dina Marios.

No comments: