Shoga kuwa waziri
wa mambo ya nchi
za nje Ujerumani
Ulaya huenda ikapata waziri wa kwanza shoga wa mambo ya nchi za nje, iwapo Waziri Mkuu wa Ujerumani (Kansela) Angela Merkel atakapounda serikali ya mseto, atamchagua shoga Guido Westerwelle kutoka chama cha FDP (Freie Demokratische Partei). Bi. Merkel anakitegemea chama cha FDP; kuunda mseto atakaouongoza.
Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa kwa Guido kuwa waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani kunaweza kuleta mushkeli kidogo inapohusu nchi za Arabuni, Mashariki ya Kati na ya mbali; sehemu ambazo ushoga na usagaji ni vitu haramu. Wachunguzi wengine wanasema; ushoga wa Guido si kitu; ila hana uzoefu siasa za mambo ya kimataifa.
Juzi alipohojiwa na BBC aliwashangaza Waingereza aliposema kuwa: Uingereza mtu anatarajiwa kuzungumza Kiingereza, lakini hapa Ujerumani tunazungumza Kijerumani. Aliwajibu BBC kwa Kijerumani.
No comments:
Post a Comment